Gaza waniliza machozi!!

Gaza waniliza machozi!!

Kjnne46

Member
Joined
Dec 4, 2006
Posts
69
Reaction score
2
Machozi Yanatiririka, GAZA Waniliza
Kila Leo Nikiamka, Wewe Maskini Nakuwaza
DAMU Inavyomwagika, Yahudi Anakumaliza
Mwili Wangu Unatetemeka, GAZA Waniliza!

Mizinga Inaporomoka, Nchi Yako Kuiteketeza
Israili Njama Kazipika, Sasa Ndio Inatekeleza
Ukanda Wote Unawaka, Maiti nyang’anyang’a GAZA
Simanzi Nzito Imenivika, Nashindwa Yahudi Kumlipiza!

Roketi Mgogoro Kuzuka, Katu HAMAS Hawakuanza
Zinapoangukia Hawajafika, Waandishi Yahudi Kawakataza
Ukweli Umethibitika, Yahudi Ndie Mwarabu Kamchokoza
GAZA Yote Imeathirika, VIFO Tele VILIO na GIZA!

Ajabu Matamshi ya Amerika, Bush Eti Kutangaza
Lawama HAMAS kumpachika, Huku Israili Anampongeza
Anayeua Watoto na Vizuka, Kadamnasi GAZA Kuiangamiza
Yaashiria Ajenda Walisuka, Azma Ndio Wanaitimiza!

Chonde Chonde Mwogopeni RABUKA, Hasira Israili Punguza
Utaua Halaiki Utasumbuka, Amani ni Nyote Kuzungumza
Hata Ushindi Ukiibuka, Bado HAMAS Hujawaweza
Hamasa Mpya Watahamasika, Kuidai Tena Yao GAZA!

Suluhisho Lahitajika, Pande Zote Kuzituliza
Mapigano Yaachwe Haraka, Ulimwengu Vita Kukataza
UN na Wote Washirika, Wawe Mstari wa Kwanza
Majeshi Palestina Kuyaweka, Kuwalinda Wao na Wenza!

Mengineyo Nachelea Kuandika, Gugumizi Kinywa Kimekaza
Nionapo Maiti Kama Taka, Zimezagaa Mitaani GAZA
Ntima Wataka Kutoka, Ni Imani tu Najikaza
Mola Nijaalie Malaika, Waimarishe Nguvu Nilizosaza!


YA-ILLAHI MTUKUKA, WAPE NUSURA WANA-GAZA
DUA YETU IKISIKIKA, MIOYO TAWFIQ UTATUJAZA
YA-KARIMA YA-MALIKA, YA-HAFIDHA YA-‘AZIIZA
NURU YAKO KUMULIKA, IONDOE GIZA YA MAUTI GAZA!!

A A M I I N ! A A M I I N !!
 
Why dont you cry for Congo,Sudan,Zimbambwe,even Tanzania Albino are killed every day,kitu gani kikutoe machozi au kwa sababu wao ni wa-arabu????
 
Muulize,ndo maana tunadharauliwa kutokana na madhaifutulionayo kama huyo anayetokwa na machozi, hao watu wenye maendeleo waache wachapane tena sana,maana wao wakichapana watataka dunia yote ijue wakati sisi tukichapana wao huwa hawajali wanaangalia rwanda walikufa more than milion,same to congo hao unao walilia hawatoi msaada kamwe kwa congo tena ndio wanafurai maana wanapata silicon nk.Tena hao gaza wachapwe tu wamezidi ubabe kwanini wanarusha maroketi kuua raia wa israel acha na raia wa gaza wafe kama wenzao wa israel.
 
Why dont you cry for Congo,Sudan,Zimbambwe,even Tanzania Albino are killed every day,kitu gani kikutoe machozi au kwa sababu wao ni wa-arabu????

ALIFU: Jibu liko katika Shairi lenyewe, kwani fumbo mfumbie mjinga .......

BAA: Kuomboleza, kushangilia ama kushabikia kitu sio lazima kiwe nyumbani kwako, nchini mwako au jirani yako. NI UAMUZI WA MTU MWENYEWE kama vile walivyo baadhi ya wana-JF wanashabikia Arsenal, Barca au MAN U na KUIPONDA TAIFA STARS lakini siwalaumu au kuwauliza kulikoni "ingawa mimi sipendezwi na jazba yao".

TAA: Nimewaita Waarabu kwa sababu ndio walivyo (sio Wazungu au Wafrika) na HAMAS ni chama chao cha ukombozi cha kumtoa mvamizi (Yahudi) anayeikalia nchi yao kwa mabavu. Ingawa Hamas walishinda kura katika Uchaguzi wa Palestina bado wanaitwa "terrorists" kama vile jina la Mandela bado limo katika orodha ya FBI ya Magaidi! Hizo njama zote tunazifahamu.....

THAA: Kwa upande wangu, hii ni tamati ya mada hii. ALAMSIKI!!
 
Why dont you cry for Congo,Sudan,Zimbambwe,even Tanzania Albino are killed every day,kitu gani kikutoe machozi au kwa sababu wao ni wa-arabu????

That's right! Mtu hawezi kulilia damu ya mbali na akashindwa kulilia ya karibu. Yaani anaonyesha huruma mbali kuliko ndugu zake wanaokufa kila siku ama kwa sababu ya hali yao ya maisha, rangi ya ngozi yao, mali au sababu ya kukosa huduma bora za kijamii hapa nchini?
 

Is this an international news or ni nyimbo za taarabu? People, let us be serious.

Mods, peleka hili shairi kwenye jukwaa husika.

Hili shairi linatia kichefuchefu
 
Back
Top Bottom