Gazeti la Jitambue

Nchaby

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
797
Reaction score
259
Habari za weekend wanajamvi. Kunako miaka ya 1990s kulikuwa na gazeti pendwa lililokuwa likijihusisha na masuala ya sayansi na saikolojia ya binadamu likifahamika kwa jina la JITAMBUE.

Hili gazeti lilikuwa likieleza namna akili ya binadamu ilivyo na nguvu ya ajabu ya kuweza kutoa majibu ya kitu anachowaza binadamu na kueleza sayansi ambayo wanasayansi bado walikuwa hawajaweza kuielezea ipasavyo.

Nilikuwa nikilipenda sana hili gazeti ambalo likuwa likitolewa kila siku ya jumatano. Sikufahamu aliyekuwa analimilki gazeti hilo, na sijui lilikopotelea.


Wanajamvi kama kuna yeyote mwenye chohote juu ya gazeti hilo anijuze.
 
Mungu amlaze pema Munga Tehenan. Lile gazeti lilikuwa si mchezo.

cc Mtambuzi. Fufua hili gazeti mkuu. Tutakusapoti.
 
Last edited by a moderator:
R.i.p Munga Tehnan..uliyatenda vema yakupasayo kipindi ukiwa dunian.
 
Nilikuwa mdogo sana wakati wa gazeti hilo.....wala nlikuwa silielewi
 
Mungu amlaze pema Munga Tehenan. Lile gazeti lilikuwa si mchezo.

cc Mtambuzi. Fufua hili gazeti mkuu. Tutakusapoti.

R.i.p Munga Tehnan..uliyatenda vema yakupasayo kipindi ukiwa dunian.

Huyo MUNGA TEHENAN inaonekana alikuwa mtaalamu sana aliyebobea mno katika masuala ya saikolojia. Alivyokufa tu na gazeti likafa! R.I.P. TEHENAN, sikuwa najua kama hatunaye huyo gwiji.


Kuna yeyote anaejua taaluma ya huyo gwiji late TEHENAN?
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa mdogo sana wakati wa gazeti hilo.....wala nlikuwa silielewi
Sema labda hauna tabia ya kusoma magazeti. JITAMBUE na gazeti ndugu yake MSHAURI WAKO, yalikuwepo hadi mwaka 2008.

Pia alikuwa na kipindi TVT na miaka ya 2003-2005 alikuwa akitoa mihadhara pale ukumbi wa Nkrumah UDSM kila J'mosi.

Baada ya Munga Tehnan kufariki, na gazeti likafa.
 
Dah. Masikini, Tanzania tunahitaji vitu kama hivi, vina add-value kwenye maisha ya jamii.

Mi sidhani kama nimeona hili gazeti
 
..mi nilibahatika kupata nakala mbili sikumbuki ni lini ila nilichokisoma mule kilinisisimua sana mpaka leo nakumbuka,sijawahi soma gazeti kutoka Tanzania lenye "vitu adimu"kama JITAMBUA.yule jamaa alistahili pongezi za pekee..
 
Nilikuwa mdogo sana wakati wa gazeti hilo.....wala nlikuwa silielewi

Mdogo sana ukimaanisha umri gani? Mi nikiwa darasa la nne nlikuwa msomaji mzuri tu wa magazeti. Labda unambie 2008 ulikuwa la kwanza, au huko ulipokuwepo magazeti yalikuwa hayafiki.
 
Nakumbuka baba yangu alikuwa anafanya kazi kwenye hayo magazeti ya jitambue. Kila jioni ikifika wanakuja home,geti linafunguliwa gari(pick up) linaingia ndani na mzigo wa magazeti then wanashusha wanaingiza ndani halafu kesho asubuhi wanayachukua wanaondoka. By that time nlkuwa mdogo i think kitu kama nursery/darasa la kwanza hivi but i could read their titles.
 
Last time mimi nimesoma gazeti la jitambue mwaka 2008 nililipenda sana bahati mbaya lilipotea hafla
 
mh sidhan km limeanzishwa miaka hyo hiv halijaanza miaka yaa 2000?sikuwah kukosa nakala zake na had mwaka jana nilikua na nakala zakenilizitunza kwl kweli,mimi lile gazeti lilinibadilisha maisha yangu kwa 99%mkewe nilikua naonana nae sehem za tegeta namuuliza anasema litarudi yaan niliumia sana kusikia kifo cha TEHENAN jman,
lilikua linafumdisha mambo meng jins ya kujitambua na ngv uliyonayo ndani ya mwili wako...dah wema wanakufa wanabaki wabovu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…