Tetesi: Gazeti la 'Mbongo' huenda likauzwa au kufungwa wiki ijayo..

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Ikifika wiki ijayo kuanzia Jumatatu nitafafanua kwa kina zaidi.

Kuna taarifa kwamba mmiliki wa gazeti 'Mbongo' amekuwa kwenye majadiliano na makubaliano ya mwisho wiki hii (sijui ya lazima au hiari) kuhusu uwezekano wa kununua gazeti lake au kufungwa kwa maslahi mapana ya GS ijayo.

Mwenyekiti anategemea vyombo vya habari vitamsaidia kufanya Promo hivyo mkakati uliopo ni kuvinunua vyote au kuvifungia mpaka upepo huo upite.

Gazeti "Mbongo" lipo kwenye hatua za mwisho kuwa mali za chama rasmi baada ya Ch10 na Maajabu ef'em!
 
Interest si ungetutolea na mtihani kabisa wana JF, maana umeandika kwa MAFUMBO na VITENDAWILI visivyojibika kwenye huu uzi wako.[emoji2955]
 
"Mtanzania" ina shida sehemu
 
Napendekeza serikali iajiri wahariri wake katika vyombo vyote vya habari.
Hii itaepusha habari isiyotakiwa kuruka
 
What is GS?
 
Mwenyekiti anatapatapa Atatangazwa na matendo yake magazeti ni makaratasi tu
 
mbona Mtanzania wametangaza wenyewe kwamba ugumu wa maisha umesababisha kuanzia jumatatu wataacha kuchapisha gazeti lao , taarifa zipo humu jf
hii ilikuwa pre emptying, ili watu wasishangae in future actions.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…