Gazeti la Mtanzania laburuzwa Mahakamani !

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
594
Wana JF,

Assalaam aleykum !

Chuo cha kiislamu cha Al - jazeera cha jijini Mwanza kimelifikisha mahakamani gazeti la Mtanzania kikidai fidia ya shilingi Bilioni mbili kufuatia kuripoti habari kuwa chuo hicho kinaendesha mafunzo ya Ugaidi.

Gazeti hilo litokalo kila siku, limefunguliwa mashitaka na chuo hicho na kwa mara ya kwanza limefikishwa mahakamani April 30,2013 katika mahakama kuu jijini Mwanza kujibu mashtaka yanayolikabili na kuahirishwa hadi julai 16,2013.

Hata hivyo kesi hiyo imedaiwa kushindwa kusikilizwa na kulazimika Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mh Mwangesi kuihairisha kufuatia mwakilishi wa gazeti hilo jijini Mwanza kudai kuwa hakuwa na hati ya mashitaka.

Source: Gazeti la An - nuur

The Fixer,

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mmmh ndio pakutokea?

Mtanzania hata baada ya wiki mbili wameshindwa kuthibitisha wala kuwaomba radhi wamiliki wa chuo hicho na walielezwa azma ya kwenda mahakamani wakasema " all the best " !

Sasa kwanini wasishtakiweee......na habari zao za KIUCHUNGUZI !
 
"Kuihairisha" au "kuiahirisha?"
Siku hizi hata watangazaji wa Redio na TV "wanachemsha" kiswahili kweli kweli!
 
Mtanzania hata baada ya wiki mbili wameshindwa kuthibitisha wala kuwaomba radhi wamiliki wa chuo hicho na walielezwa azma ya kwenda mahakamani wakasema " all the best " !

Sasa kwanini wasishtakiweee......na habari zao za KIUCHUNGUZI !


inawezekana wana ushahidi hawawezi kuandika habari kama iliyo bila kuwa na uthibitisho
 
inawezekana wana ushahidi hawawezi kuandika habari kama iliyo bila kuwa na uthibitisho

Mkuu "Bad head " !
Hawa Mtanzania waliambiwa wathibitishe ama kuwaomba radhi tena kwa kupewa notisi ya wiki 2 na Mashahidi wao wakubwa niwapita njia ambao nadhani hata Mahakamani watawatafuta waende kuwathibitishia kuwa tuhuma zao ni za kweli !

Tusubiri.....
 
"Kuihairisha" au "kuiahirisha?"
Siku hizi hata watangazaji wa Redio na TV "wanachemsha" kiswahili kweli kweli!

Hahaa hahaha hahaahaaa !
Mkuu Buchanan, yaaani umeona neno hilo tu habari nzima hiyo ?
 
Kaufafanuzi kidogo:Mkuu The Fixer,Mtanzania hawawezi kusema hawakupata Hati ya Mashtaka.Hii ni kwakuwa shauri husika ni la madai.Watakuwa hawajapata Hati ya Malalamiko (Plaint) kama kweli hawajaipata. Shauri lenyewe litakuwa ni la Kutweza(Defamation)Pia,wako Mahakama Kuu kwakuwa shauri a thamani ya bilioni mbili haliwezi kusikilizwa Mahakama za chini: ya Mwanzo,ya Wilaya/ya Hakimu Mkazi. Mtanzania wanaweza kujinasua kama watathibitisha walichokiandika au wakithibitisha kuwa walikuwa wakitoa maoni tu au kwamba walishaomba msamaha au kwamba ni jambo linalojulikana na wote.Kila la kheri kwa pande zote za shauri.Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 

Hichi chuo kina usajili? na kinatoa kozi gani?
 

Ingia web ya nacte co kila ki2 utafuniwe!
 
Hizo habari ni za kweli na ushahidi upo sasa kama Mtanzania hawana mimi ninao .Suala la kuthibisha huwa linathibitishwa Mahakamani na Sio popote pale!!!
Nchi hii wapo watu wanafanya uhalifu kwa mgongo wa dini!!!
Ni jambo la ajabu gazeti hili limeandika na kufichua mahali alipo Shehe Illunga na kuiomba Serikali kusaidia matibabu yake na Wakabainisha kuwa Ubalozi wa Tz India ndio unaoratibu gharama zake zote lakini Waziri Nchimbi alitangaza kuwa Illunga ametoroka Sasa unadhani katika mazingira haya unataka Mtanzania wapeleke ushahidi kwa nini wakati serikali ipo hivyo ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…