Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Msemaji wa serikali: Mfano tarehe 30 Januari lilichapisha habari yenye kichwa cha habari 'Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM' ilhali ndani linazungumzia ufisadi ndani ya shirika la elimu Kibaha, ni kiwango cha juu sana cha sensetionalism. Tuliwaita wakaona udhaifu wao na kuomba Radhi na tukawasamehe.
Miezi miwili baadae April 27 wakaja na habari kubwa Mwakyembe: Maisha yangu yako hatarani. Hii stori ilikuwa ya kutunga, Mwakyembe hakuzungumza popote na mhariri wa Mwanahalisi wala mwandishi yoyote, wakaomba radhi kwenye gazeti lao la Mei kwa mheshimiwa Mwakyembe kwa kuomba Radhi, wakaahidi kwenye gazeti kuchukua hatua za kinidhani kwa mhandishi aliezusha, hatua hatujazisikia hadi leo na bado wameendelea na uandishi huo.
September 4 walikuwa na habari nyingine kubwa 'Makinikia yakwama'. Ni mfano mwingine wa habari ya kutunga, tukawapa muda wasahihishe lakini wakakataa kwa maana hawaoni kosa kisheria. Msingi wa kwanza kwenye uandishi wa habari ni ukweli, kamati ya makinikia imekwama wapi na lini, hata ukisoma Miga ina msingi wa confidentiality, sasa katikati ya mazungumzo gazeti kuibuka na kusema mazungumzo yamekwama.
========