menny terry
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 509
- 670
Wakuu,
Gazeti la Raia Mwema lilikuwa ni mojawapo ya magazeti makini sana Kwa kuandika makala yakinifu zenye kujenga sana. Ajabu ni kuwa Siku za Karibuni Kwa hali isiyokuwa ya kawaida gazeti hili Kila siku ni ku report kuhusu migogoro ya dini na madhehebu fulani.
Hakuna dini wala dhehebu lisilo na mgogoro, migogoro ni kawaida kwenye sehemu yenye mawazo Na mitazamo tofauti, lakini ajabu ni kuwa hata changamoto ndogo tu wao huikuza Na kuifanya ni boonge la habari. Najiuliza ni nini hasa ajenda ya hili gazeti?
Wamiliki wa hili gazeti wametumwa na nani? Wanafanya haya kwa faida ya nani? Hivi ni kweli hakuna habari zenye tija Kwa Taifa mpaka kila siku iwe ni Kusakama dini za watu? TCRA mko wapi? Haya mambo yakiachwa kwa muda huleta mpasuko kwa Taifa usio na sababu yoyote.
Nawasilisha.