Gazeti la Serikali “Habarileo” halijui kama Masheikh wameachiwa huru

Gazeti la Serikali “Habarileo” halijui kama Masheikh wameachiwa huru

Joined
Sep 19, 2019
Posts
43
Reaction score
383
GAZETI LA SERIKALI “HABARILEO” HALIJUI KAMA MASHEIKH WAMEACHIWA HURU

Na Sheikh Ponda Issa Ponda

Takriban Magazeti yote makubwa ya leo habari kubwa ni tukio la kuachiwa huru Viongozi wakubwa wa Dini maarufu kwa jina la “Masheikh wa Uamsho”.

Kwa namna ya pekee gazeti la Serikali halina kabisa habari hiyo katika uso wake.

Kwa mujibu wa tasnia ya habari chombo cha Habari kinapoitangaza habari mwanzo au kuiweka katika ukurasa wa mbele maana yake habari hiyo ni nzito na muhimu.

Kwa bahati mbaya au kwa hoja ya waendeshaji wa chombo hicho cha Serikali tukio la viongozi wa Dini (au Raia) kuwekwa gerezani kwa miaka minane na hatua ya Serikali (DPP) kufuta mashtaka dhidi yao si jambo zito wala muhimu la kuwekwa mbele katika gazeti la serikali.

Mimi sioni kama dhana hii ni sahihi. Nitumie fursa hii kuwashauri waendeshaji wa chombo hiki wazitakase nyoyo zao na wajilazimishe kwenda na mabadiliko ya mazingira au wakati.

Nawatakia kazi njema

0656654546.
 
Mkwere alitaka kumuua huyu mwamba hadi leo wanashangaa ile risasi ilimkosaje moyo. Huyu mwamba kitu alichopungukiwa tu ni kimoja hajamkubali YESU Mungu wa kweli.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom