Gazeti linaloongozwa na kupendwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki hatimaye limerejea mtaani baada ya kukaa nje kidogo ya ulingo kutokana na kutoa taarifa iliyokuwa haina usahihi.
Taarifa za awali zinadai katika baadhi ya vituo vya wauza magazeti katikati ya jiji, nakala ziliisha kuanzia saa 12, huku maeneo ya Mbezi stendi watu wakipanga foleni kupata kopi na maeneo ya Karume watu walionekana kugombana ili kupata nakala moja iliyokuwa imebaki.
Kifungo cha muda mfupi (mbwa kala mbwa). Sipati picha lingekuwa gazeti la Mwananchi, Raia Mwema, Mawio! Uhuru imerudi mapema ili kuendelea kueneza propaganda za kijani kibichi...