Gazeti la Uwazi Lachapia

Gazeti la Uwazi Lachapia

Mnhenwa Ndege

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2007
Posts
242
Reaction score
21
Picture+023.jpg

Inasikitisha kuona gazeti kama Uwazi linachapia pale wanapotoa picha ya Randy Jackson wa American Idols kudhani kuwa ni Randy Jackson mdogo wake hayati Michael Jackson. Randy Jackson wa American Idols mara nyingi alikuwa anasema kuwa yeye ahusiani na Michael Jackson ni majina tu yamefanana, pia kiumri amemzidi Michael jackson kwa kuwa yeye kaziliwa 1956 wakati Randy Jackson mdogo wake Michael alizaliwa 1961.

Picture+024.jpg

Gazeti hili pia lilichapia walipotoa picha ya Randy Jackson wakisema ni Tito Jackson ambaye ni kaka ya Michael Jackson. Kwa kifupi gazeti hili haliko makini ukilisoma lazimi uthibitishe yaliomo. Labda pengine kuna mtu sasa hivi akiangalia American Idols anaweza kubisha kuwa Randy (jaji wa shindano hilo) ni mdogo wa Michael Jackson kumbe hawana undugu.

Source: Pwani Raha Blog
 
Hawa ni kawaida hawana tofauti na zeuchungu.
 
Makubwa, wanashindwa hata kutafuta facts kwenye tabloids basi!, kama hawawezi kufanya homeworks zao vizuri.
 
Wamezoea kukurupuka wakidhani ndo wajuaji zaidi.mbaya zaidi hawataomba msamaha kwa kudanganya umma!!
 
Back
Top Bottom