Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Bila ya Salamu.
Mwanasimba kindakindaki na mmoja wa viongozi waandamizi wa Tawi la Simba SC katika soko la Karume ametoa tathmini nzima ya usajili wa klabu ya Simba katika dirisha hili kubwa la Usajili kuelekea msimu mpya wa 2024/2025.
Gb64 ni miongoni mwa wasemaji fasaha katika wanachama wa Simba SC, mwenye uwezo wa kuvuta maelfu ya mashabiki wakakaa chini na kumsikiliza amesema kwa wachezaji wapya wanaosajiliwa na Simba wanahujumiwa kwa kufanyiwa vitendo vya kishirikina pindi wanapofika Simba sc. Sio kwamba hawana viwango bali viwango vyao vimekuwa vikidhohofishwa kwa ulozi unaofanywa na watani wa jadi wakishirikiana na mapandikizi yao yaliyojificha ndani ya klabu ya Simba sc.
Ametoa wito kwa uongozi wa klabu kuhakikisha wanawalinda wachezaji vya Visomo vya dua na maombi mbalimbali ili vitendo hivyo vya kishirikina visiweze kuwadhuru wachezaji wetu.
Pia ameupongeza uongozi wa Simba ukiongozwa na tajiri kijana, Mheshimiwa Rais Mohammed Dewji aka Mo kwa kuweza kuondoa magugu yaliyoota ndani ya Simba na kuleta wachezaji wenye umri mdogo na viwango vikubwa barani Afrika.
Pia amedokeza kuwa kuna sajili mbili kubwa zinasubiriwa kutangazwa na Simba ambazo si nyingine bali ni yuleyule Zanzibar finest, FEI TOTO na Mshbuliaji Elia Mpanzu.
Mwisho amemaliza kwa kusema kuwa mechi ya ngao ya jamii inakwenda kuwa ni mechi ya KAZI na UMRI. Mechi baina ya damu changa na wachezaji waliotelekezwa na kuishia kuokotwa na watani wa jadi.
Source: SportsMax