LGE2024 Geita: ACT Wazalendo waitupia lawama CCM changamoto za Uchaguzi

LGE2024 Geita: ACT Wazalendo waitupia lawama CCM changamoto za Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Geita, Lucas Tibengana amesema kuwa zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa limekumbwa na changamoto kutokana na mfumo wa majina, hali Iliyosababisha baadhi ya wananchi kushindwa kushiriki katika upigaji kura.

Akizungumza katika kituo cha kupigia kura kilichopo mtaa wa Mwatulole, kata ya Buhala Hala, Tibengana amedai kuwa wagombea wa chama chake waliondolewa majina yao bila sababu za msingi, huku akielekeza lawama zake kwa Chama Cha Mapinduzi, akidai chama tawala kilihusika katika kuwatenga baadhi ya wagombea wa upinzani.

Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita, Gabriel Nyasilu amekanusha madai hayo, akisisitiza kuwa vyama vyote vilipata nafasi ya kukata rufaa kabla ya uchaguzi.

“Serikali ilitoa muda wa kutosha kwa vyama vyote kuwasilisha rufaa kwa wagombea waliodai kuonewa. Kilichobaki ni malalamiko yasiyo na msingi ambayo yanaweza kuwachanganya wananchi,” ameema Nyasilu.

Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi wa halmashauri ya Mji wa Geita, Yefred Miyenze amesema kuwa hakuna changamoto kubwa iliyojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

“Madai haya ni jitihada za baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwapotosha wananchi. Uchaguzi umeendelea bila matatizo makubwa,” amesema Miyenze.

PIA SOMA
- LGE2024 - ACT Wazalendo: Wagombea wetu 51,423 wameenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
 
Back
Top Bottom