Geita: Amsababishia mwenzake kifo wakati akimtoa mimba nyumbani

Geita: Amsababishia mwenzake kifo wakati akimtoa mimba nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, linamshikilia Vestina Michael (44), mkazi wa Buseresere wilayani Chato kwa tuhuma za kumtoa mimba na kumsababisha kifo Mariam Msalaba (40), ambaye alipoteza maisha muda mfupi baada ya kutolewa mimba nyumbani kwa mtuhumiwa.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Henry Maibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kitendo hicho cha kikatili kimetokea nyumbani kwa mtuhumiwa majira ya usiku.

"Jeshi la Polisi tunamshikilia Vestina Michael, kwamba siku ya Oktoba 31 mwaka huu marehemu alifia nyumbani kwake na ndugu wa marehemu wakaleta malalamiko kwamba, ndugu yao amefia kwa mtuhumiwa wakati akimtoa mimba, hivyo tunamshikilia huyo mtuhumiwa", amesema Kamanda Mwaibambe.
 
Duh si angezaa tu huyo mtoto maana ni mtu mzima au atumie dawa za uzazi, apumzike panapomstahili
 
[emoji44][emoji44][emoji44].hao mbona ni wazee kabisa
Au huyo mwanamke ni mwanafunzi
 
mbona hamsemi kua mtuhumiwa alikua ni diwani mteule wa sisiemu?
 
Pole yao sana wfiwa... Sheria ifuate mkondo wake, baada ya uchunguzi...




Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom