Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), limelaani vikali hatua ya kuenguliwa kwa wagombea wa CHADEMA katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Kaimu Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa, Sharifa Suleiman, alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake mkoani Geita, iliyolenga kuimarisha Baraza hilo. Akizungumza katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa BAWACHA mkoani humo, Sharifa alisema wanawake hawatarudi nyuma katika kushiriki uchaguzi huo.