Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Picha: Sehemu ya maduka iliyoathirika
Maduka 16 ya wafanyabishara wa soko la CCM kakubilo lililopo katika Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani Geita yameungua kwa moto juzi usiku kuamkia jana na kuteketea kabisa.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Geita, Wilson Shimo imefika katika eneo hilo na kujionea hali halisi huku maduka 16 yakiwa yameungua na baadhi ya vitu kuibiwa baada ya moto huo kutokea na chanzo chake bado hakijajulikana.
Aidha Shimo ameliagiza Jeshi la polisi kwa kushirikiana na uongozi wa soko hilo pamoja na viongozi wa kata kuhakikisha wanashirikiana kuwasaka wote waliokwenda kutoa msaada na kuiba mali ambazo zilikuwa hazijateketea kuondoka nazo kusiko julikana.
Chanzo: Star TV