Pre GE2025 Geita: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Geita: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Geita. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

1729461354045.png
Mgawanyiko wa Idadi ya Watu kwa Majimbo ya Uchaguzi Mkoa wa Geita; Ramani ya Sensa ya Watu na Makazi ya 2022

Mkoa wa Geita upo Kanda ya Ziwa katika Tanzania na ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji, pamoja na madini, hasa dhahabu. Mkoa huu una historia ya utajiri wa madini, hususan kupitia mgodi maarufu wa Geita Gold Mining.

Idadi ya Watu

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Geita ni watu 2,977,608; wanaume 1,463,764 na wanawake 1,513,844.

Mkoa huu una Halmashauri sita (6) na majimbo saba (7) ya uchaguzi ambapo Jimbo la Busanda linaongoza kwa kuwa na watu wengi (671,761) likifuatiwa na Jimbo la Chato (watu 584,963). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Jimbo la Nyang'hwale ambalo lina watu 225,803, huku ukiwa na wilaya 6.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi

Mkoa wa Geita una jumla ya majimbo 7 ya uchaguzi:
  • Jimbo la Geita Vijijini
  • Jimbo la Busanda
  • Jimbo la Geita Mjini
  • Jimbo la Nyang'hwale
  • Jimbo la Mbogwe
  • Jimbo la Bukombe
  • Jimbo la Chato
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Mkoa wa Geita ulishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi zaidi kulinganisha na wapinzani wake.

Katika uchaguzi wa Ubunge, wagombea walishinda kwa kishindo kwa kura nyingi, huku wengine wakipita bila kupingwa na CCM kujinyakulia majimbo yote.

Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kwa kishindo. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu kutokuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi.

Updates

January
  1. Pre GE2025 - Stephen Wasira Amjibu John Heche Kuhusu Umri Wake Mkubwa. Asema Gari ni Injini Na Siyo Bodi
  2. Pre GE2025 - Wassira: Maridhiano ni lazima, nchi nyingi za Africa zilipitia Mapinduzi ya Kijeshi Lakini Tanzania tumekuwa Kisiwa Cha Amani!
  3. Pre GE2025 - Wassira: Wanaosema CCm imekaa sana walikuwa wapi wakati tunadai uhuru
  4. Pre GE2025 - Wassira: CCM ni chama kikubwa hakiwezi kuamrishwa na 'Kibaka'
  5. Pre GE2025 - Wasira: Mabeberu na Vibaraka wao wanataka kuleta Ushoga
February
March


ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom