LGE2024 Geita Mjini: CHADEMA walalamikia kuenguliwa kwa wagombea Uchaguzi Serikali za Mitaa

LGE2024 Geita Mjini: CHADEMA walalamikia kuenguliwa kwa wagombea Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Mambo ni moto kila sehemu, ni mwendo wa kuengua tu na kubakisha wa kupita bila kutoa jasho.

=====


Viongozi na Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Geita Mjini mkoani Geita, wamelalamikia kuenguliwa kwa majina ya wagombea wao wa nafasi za Uenyekiti na Ujumbe katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kufika kwenye ofisi za Serikali ya mtaa wa NMC, Kata ya Kasamwa kwa ajili ya kufikisha malalamiko yao, Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Geita Mjini Pasiquna Lucas amesema miongoni mwa sababu zilizopelekea kuenguliwa kwa wagombea wao ni makosa katika ujazaji wa fomu.

Hata hivyo, alilalamika kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vingine wamepitishwa licha ya kuwa na mapungufu mengi.
 
my lady,

hiyo imeisha,

wajipange tu kwaajili ya chaguzi nyingine, na wazingatie kanuni, sheria na katiba ya nchi kuhusu uchaguzi husika. Malalamiko si kitu cha maana sana kama wagombea hawana sifa na hawajajiandikisha kupiga kura :pulpTRAVOLTA:
 
Aonyeshe ushahidi hadharani waliopitishwa wakiwa na mapungu ili twende sawa biashara ya kulishana matango pori haifai, weka form zao hapa hadharani, hata za kufoji tu,ili tujiridhishe
 
Back
Top Bottom