Geita: Mke ajinyonga Kisa kushutumiwa kuiba elfu kumi ya mumewe

Geita: Mke ajinyonga Kisa kushutumiwa kuiba elfu kumi ya mumewe

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Kama kawaida Geita hakupoi..

Mke ajinyonga Kisa kushutumiwa kuiba 10,000 ya mumewe👇
---
1663250387973.png

Picha: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi (ACP), Henry Mwaibambe

ASIA Kibishe (27) mkazi wa Kijiji cha Nyarututu, Kata ya Bwanga, wilayani Geita amekutwa amejinyonga, chanzo kikidaiwa ni kutuhumiwa kuiba Sh 10,000 ya mumewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi (ACP), Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, mapema mwezi huu saa 1;30 asubuhi.

Kamanda Mwaibambe amesema marehemu alikutwa amejinyonga kwa kutumia kipande cha kanga, ambapo marehemu mwili wake ulikutwa unaning’inia kwenye mti karibu na nyumbani kwao.

“Chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati yake na mme wake aitwaye Fabian Shija (23), ambaye ni mkulima na mkazi wa kijiji hicho cha Nyarututu, kwamba alikuwa anamtuhumu marehemu kumuibia Sh 10,000 iliyokuwa chumbani kwao,” amesema Kamanda huyo.

Pia amesema Jeshi la Polisi limsaka mtu mmoja kwa tuhuma za wizi wa mtoto aitwaye Evance Joseph, mwenye umri wa miezi sita na juhudi zinaendelea kumpata mtoto na mtuhumiwa.

“Mnamo Septemba 3, 2022 majira ya saa saba mchana huko kijiji na kata ya Lulembela tarafa ya Ilolanguru wilaya ya Mbogwe, mama wa mtoto aitwaye Magreth Joel (23), aliripoti kuibiwa mtoto wake huyu,” amesema Kamanda.

Chanzo: Habari Leo
 
Kama kawaida Geita hakupoi..

Mke ajinyonga Kisa kushutumiwa kuiba 10,000 ya mumewe👇
Recap
  1. Katekista abaka mtoto wa miaka 8
  2. Mlinzi ampiga risasi aliyetaka kumkata na shoka
  3. Mke ajinyonga kisa kusingiziwa kaiba 10K
Anyway sasa mume ajaribu kuwasaka panya huenda wamejengea kiota
 
Daah watu wanafua wakiona pesa kwenye mifuko ya suruali hawaridishi yeye buku 10 anajinyofoa roho aisee.
 
Aisee!! Inasikitisha sana.

Sijui huyo Mume anajisikiaje huko aliko.
 
Tatizo la afya ya Akili ni kubwa kuliko tunavyo lichukulia hapa nchini kwetu.
 
Na yeye yani kusingiziwa hilo tuu ndo ajiue
 
Back
Top Bottom