GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Sipajui sana Geita, lakini napafahamu, alau kidogo. Habari zake zimevuma ndani na nje ya Tanzania, hasa kwa shughuli za "uvunaji" dhahabu!
Hivi karibuni, nimesimuliwa kuwa baada ya Mzungu mmoja huko ughaibuni kukutana na dhahabu iliyodaiwa kuwa ilichimbwa na kampuni ya Geita Gold Mine (GGM), iliyopo Geita, aliamua kufungua safari hadi Geita nchini Tanzania. Alitaka kwenda kujionea ustawi wa mji ulikotoka hiyo dhahabu! Alichokiona ni tofauti na alichokitarajia.
Kwa "madhahabu" yanayozalishwa Geita, alitarajia kukuta maskycraper ya maana, kumbe hakukuwepo hata na ghorofa lenye lifti.
Alitarajia kukuta maflyover mengi, lakini kumbe hata barabara zenye lami ni chache mno.
Alitegemea kukuta mji uliojengwa ukajengeka, matokeo yake alikuta kuna mpaka nyumba za nyasi.
Alifikiri, kama vile Almasi ilivyosaidia kuijenga Afrika Kusini, na dhahabu nayo itakuwa imeisaidia Geita kuwa jiji la kipekee sana.
Geita ina "madhahabu" mengi mno. Ni kati ya mikoa ambayo machimbo ya dhahabu yanaendelea kuibuliwa na raia wa kawaida. Si mara moja wala mbili, mtu amebadili "plan" ya kuchimba shimo la choo baada ya kukutana na mwamba wenye dhahabu, na kupelekea shimo lililokusudiwa kuwa la choo kugeuka kuwa mgodi wa dhahabu.
Takwimu za mwaka 2020 zinaonesha kuwa Geita, mkoa "mtajiri" wa dhahabu, unazidiwa na mkoa wa Lindi kwa utajiri. Sijui hilo limekaaje! Labda Wachumi watanisaidi.
Geita, mkoa "mtajiri" kiasi hicho, unakosaje kuwa na stendi ya kisasa?
Geita, mkoa "mtajiri" wa dhahabu, unapitwaje kwa utajiri na mkoa wa Iringa ambao Mhe. Dr. J. K. Msukuma aliuita ni mkoa wa walima nyanya?
"Nimepita" Iringa, na nimekaa kwa muda mkoani Geita. Naam, hata sasa ninapouandika huu uzi, nipo Mkoani Geita. Kwa mwonekano tu, Iringa panaonekana pameendelea sana ukipalinganisha na Geita.
Kwa nini Geita mkoa "mtajiri" siyo tajiri?