Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mapenzi na migogoro ya ndoa imeendelea kuleta shida na hata kutoa roho za watu kila kukicha jamaani!
==================
Mwanamke mmoja mkazi wa kata ya Ludete wilayani Geita, Adventina Nicolaus (37) amefariki baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mume wake, huku tukio hilo likihusishwa na mgogoro wa kifamilia.
Inaelezwa kuwa tukio hili limetokea usiku wa kuamkia Januari 7, 2025.
Kwa mujibu wa mashuhuda na ndugu wa marehemu, mtuhumiwa alitekeleza kitendo hicho na baadaye kuwapigia simu ndugu wa Adventina kuomba msamaha kwa kile alichokitenda.
Soma Pia: NJOMBE: Amkata Mume wake sehemu za Siri ya kubaini anachepuka nje
Yasinta Nicolaus, mdogo wa marehemu na Elizabeth Nicolaus, pia mdogo wa marehemu wameeleza kushtushwa na msiba huo wa ghafla.
Baadhi ya majirani wa familia hiyo wameonyesha masikitiko yao makubwa kuhusu tukio hilo na kulaani vikali kitendo cha kuua, wakieleza kuwa, hata kama kunatokea kutokuelewana kati ya wanandoa, suluhu inapaswa kutafutwa bila kutumia nguvu au kujichukulia sheria mkononi.
Adventina Nicolaus ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka miwili. Jamii na mamlaka zinahimizwa kushirikiana kuhakikisha haki inapatikana na matukio ya aina hii