"Uchaguzi huu tuufanye kwa amani na utulivu, aliyeshinda atangazwe na ambaye hajashinda asitangazwe. Niwaombe watu wote waliojiandikisha wasiache kuja kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua kiongozi wanaemtaka ili tuweze kusukuma mbele maendeleo yetu.
Tunataka Kiongozi ambaye atazungumza shida za watu, kiongozi ambae atajishughulisha na matatizo ambayo watu wanayo kwenye vitongoji vyao, tunatamani tupate Viongozi ambao kazi yao kubwa haitakua tu kupata vyeo vya kujitambulishia, iwe ni kazi ya kupata cheo kwaajili ya kufanya kazi ya Watu" Dkt. Biteko