Geita: Watu 6000 wavamia nyumba ya mtu ili kuchimba dhahabu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
ENEO la nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Nyambogo Kata ya Nyakafuru Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita limevamia na watu zaidi ya 6,000 kwa ajili ya kusaka madini ya dhahabu.

Makundi mbalimbali ya watu kutoka maeneo kadhaa yamefika kijijini hapo kwenye nyumba hiyo, baada ya mwanakijiji mmoja aliyekuwa akichimba choo kupata dhahabu.

Imeelezwa kuwa mwanakijiji huyo wakati akichimba choo nyumbani kwake kabla hakijawa na kina kirefu, aliufikia mwamba unaosadikiwa kuwa na dhahabu ndipo aliupasua na kuondoka na vipande vya mawe kwenye viroba na kuvipeleka katika mwalo wa kuchenjua dhahabu na kupata dhahabu nyingi.

Baada ya kupata dhahabu alilizungushia eneo lake na kuendeleza na uzalishaji wa madini hayo ndipo wanakijiji wenzake wakagundua kuwa mwenzao amepata dhahabu, hivyo umati ukaanza kufurika na kuanzisha uchimbaji na wanapata dhahabu na kuendeleza shughuli hizo bila kujali ni kuwa ni eneo la makazi.

Diwani wa kata hiyo, Paul Ngusa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaambia waandishi wa habari waliofika eneo la tukio kuwa baada ya madini hayo kupatikana katikati ya makazi ya mwanakijiji huyo katika choo kilichokuwa kikichimbwa, uongozi wa serikali uliwafuata wamiliki wa maeneo yote ya jirani na mkazi huyo kuwaeleza fursa ya uwapo wa dhahabu kwenye makazi yao.

“Baada ya fursa hii ya kupatikana kwa dhahabu kwenye maeneo ya wakazi wa Kijiji cha Nyambogo kutokana na mmoja wao kuigundua wakati akichimba choo, tumekaa nao na tumekubaliana kwamba wataondoka kwa hiari yao ili kupisha shughuli za uchimbaji wa madini hayo,” alisema diwani huyo na kuongeza:

“Lakini wenye maeneo watapewa kipaumbele kusimamia maeneo yao wakati uzalishaji wa dhahabu ukiendelea.”

Alisema kuwa kama diwani hataridhika wananchi hao kukubali kuachia maeneo yao kwa ajili ya uchimbaji huo kwa maneno pekee, bali atahakikisha wanaandikishana ili kukwepa lawama hapo baadaye na baadaye muhtasari huo watamkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Charles Mabeho.

“Niseme tu kuwa mimi binafsi nimefurahi sana kupatikana neema ya uwapo wa madini kwa wananchi wangu wa Kijiji cha Nyambogo,” alisema.

“Fursa hii itasaidia kuendelea kutatua changamoto za kata nzima ya Nyakafuru ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, madawati pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara,” alisema Ngusa.

KAULI YA DC

Awali DC Mabeho akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya wilaya hiyo, alisema wiki iliyopita mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyambogo Kata ya Nyakafuru ambaye hakumtaja jina, alipata dhahabu wakati akichimba shimo kwa maandalizi ya ujenzi wa choo katika makazi yake.

“Kwenye wilaya yangu kuna fursa nyingi za maendeleo, juzi tu nina taarifa za mwananchi mmoja wa Kijiji cha Nyambobo kuwa amepata dhahabu wakati akichimba choo,” alisema na kuendelea:

“Kwa sasa mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tunajipanga kutembelea eneo hilo ili tuwe na majibu kamili.”

1630393408554.png

Chanzo: Nipashe
 
Maeneo ya vijiji hasa mkoa wa Geita yamejaa dhahabu sema tu technology ya kugundua sehemu yalipo ni duni.
Yaligundulika shamba la jirani nikajua mchirizi wa dhahabu utafika kwenye shamba letu ili nasi tutoboe kimaisha chakushangaza yalipotea ghafula
 
Pia wataalamu wa kuhamisha wapo
 
Lololo bahaati..Lololo bahaati...Lololo bahaati ya mtu mwenye shambaaa..akatupa jembe upande akaenda mjinii ..akanunua gari yake sasa ni tajiriíii[emoji3][emoji3][emoji3][emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Mmnenokumbusha enzi za ugali wa bure
 
Angeuza nyingi na kufuatilia vibali amiliki eneo loteyeye

Angeuza nyingi na kufuatilia vibali amiliki eneo lote yeye
Si rahisi kama unavyofikiria huwa iko hivi ukiwa unachimba kusima au choo au shimo la taka ukaibuka na mawe ya dhahabu inabidi uende kuyauza sehemu unayoenda kuuza lazima watu waanze kukuuliza umeyatoa wapi ukificha wanatengeneza intelligence ya hatari maana ile ni mali aisee hawawezi kukuacha utaficha siku mbili tatu wanafika wazee wa kazi kuna watu huwa wananusa dhahabu balaa maana wengine huoteshwa na waganga kabisa.
Na wakivamia usidhani Watachimba pembeni hilo sahau anachimba pembeni yako mita kazaa chini then anapiga horizontal kuja kwenye shimo lako chapuchapu yaani unaweza shangaa ndani ya dakika 10 kule chini mashimo zaidi ya kumi wameshakutana na kutengeneza ukumbi yaana biashara ya dhahabu si mchezo.
 
NAKWAMBIA NAUZA NAPIGA UKUTA NA NAFANYA SIRI SIUZI MOAKA NIWE NA TANI YA DHAHABU[emoji28][emoji23][emoji1787][emoji23][emoji28]
 
ENEO la nyumba ya mkazi wa Kijiji cha Nyambogo Kata ya Nyakafuru Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita limevamia na watu zaidi ya 6,000 kwa ajili ya kusaka madini ya dhahabu.

Makundi mbalimbali ya watu kutoka maeneo kadhaa yamefika kijijini hapo kwenye nyumba hiyo, baada ya mwanakijiji mmoja aliyekuwa akichimba choo kupata dhahabu.

Imeelezwa kuwa mwanakijiji huyo wakati akichimba choo nyumbani kwake kabla hakijawa na kina kirefu, aliufikia mwamba unaosadikiwa kuwa na dhahabu ndipo aliupasua na kuondoka na vipande vya mawe kwenye viroba na kuvipeleka katika mwalo wa kuchenjua dhahabu na kupata dhahabu nyingi.

Baada ya kupata dhahabu alilizungushia eneo lake na kuendeleza na uzalishaji wa madini hayo ndipo wanakijiji wenzake wakagundua kuwa mwenzao amepata dhahabu, hivyo umati ukaanza kufurika na kuanzisha uchimbaji na wanapata dhahabu na kuendeleza shughuli hizo bila kujali ni kuwa ni eneo la makazi.

Diwani wa kata hiyo, Paul Ngusa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwaambia waandishi wa habari waliofika eneo la tukio kuwa baada ya madini hayo kupatikana katikati ya makazi ya mwanakijiji huyo katika choo kilichokuwa kikichimbwa, uongozi wa serikali uliwafuata wamiliki wa maeneo yote ya jirani na mkazi huyo kuwaeleza fursa ya uwapo wa dhahabu kwenye makazi yao.

“Baada ya fursa hii ya kupatikana kwa dhahabu kwenye maeneo ya wakazi wa Kijiji cha Nyambogo kutokana na mmoja wao kuigundua wakati akichimba choo, tumekaa nao na tumekubaliana kwamba wataondoka kwa hiari yao ili kupisha shughuli za uchimbaji wa madini hayo,” alisema diwani huyo na kuongeza:

“Lakini wenye maeneo watapewa kipaumbele kusimamia maeneo yao wakati uzalishaji wa dhahabu ukiendelea.”

Alisema kuwa kama diwani hataridhika wananchi hao kukubali kuachia maeneo yao kwa ajili ya uchimbaji huo kwa maneno pekee, bali atahakikisha wanaandikishana ili kukwepa lawama hapo baadaye na baadaye muhtasari huo watamkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Charles Mabeho.

“Niseme tu kuwa mimi binafsi nimefurahi sana kupatikana neema ya uwapo wa madini kwa wananchi wangu wa Kijiji cha Nyambogo,” alisema.

“Fursa hii itasaidia kuendelea kutatua changamoto za kata nzima ya Nyakafuru ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, madawati pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara,” alisema Ngusa.

KAULI YA DC

Awali DC Mabeho akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya wilaya hiyo, alisema wiki iliyopita mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyambogo Kata ya Nyakafuru ambaye hakumtaja jina, alipata dhahabu wakati akichimba shimo kwa maandalizi ya ujenzi wa choo katika makazi yake.

“Kwenye wilaya yangu kuna fursa nyingi za maendeleo, juzi tu nina taarifa za mwananchi mmoja wa Kijiji cha Nyambobo kuwa amepata dhahabu wakati akichimba choo,” alisema na kuendelea:

“Kwa sasa mimi na kamati yangu ya ulinzi na usalama tunajipanga kutembelea eneo hilo ili tuwe na majibu kamili.”

View attachment 1917659

Chanzo: Nipashe
Sheria ya ardhi inakutambua wewe kama mmliki WA ardhi na maotea. Siyo madini yaliyoko chini ya ardhi
 
Back
Top Bottom