Gen.Muhoozi: Hakuna Raia Atawahi Kuwa Rais Uganda

Gen.Muhoozi: Hakuna Raia Atawahi Kuwa Rais Uganda

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take
Na ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ ilitakiwa kusema hakuna Mpinzani Atakuwa Rais bila kupepesa macho.๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Mkuu wa Jeshi la Uganda, ambaye pia ni mtoto wa kiume wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema hakuna raia atakayeiongoza Uganda kwakuwa hilo ni jukumu la wanajeshi au polisi wa nchi hiyo.

Muhoozi, ambaye amesema hatagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2026, ameandika ujumbe huo kwenye mtandao wa X kwamba wanajeshi hawataruhusu raia kuongoza Uganda.

โ€œHakuna raia ataongoza Uganda baada ya Rais Yoweri Museveni. Maafisa wa usalama hawataruhusu hilo kutokea. Rais ajaye atakuwa mwanajeshi au afisa wa polisi,โ€ ameandika Muhoozi.

Snapinsta.app_460679976_488147124139952_8075072639876587679_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom