MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
View: https://x.com/BrendaMonkango/status/1888118771555938620
Pichani(video), ni gari iliyobeba chakula kwa ajili ya wanajeshi wa jeshi la serikali ya Congo,FARDC waliopata majeraha wakati wa vita na M23. Kwa sasa, wanajeshi hao wamelazwa katika hospitali ya jeshi kwenye kambi ya Katindo huko Goma.
Mtangazaji anasema, kitendo hicho ni cha kiungwana kwa raia wenzake. Akiwa hospitalini hapo, aliweza kuongea mawili matatu na majeruhi hao; aliwatakia afya njema na kuahidi kuwa nao bega kwa bega baada ya kutelekezwa na serikali yao, na kuwaahidi pia kuwa jeshi la M23 litahakikisha wanajenga maisha yao ya badae chini ya jeshi la AFC/M23.
Ujio wake huo mbali na ubinadamu, unaonyesha nia ya AFC/M23 ya kutanguliza umoja wa raia wa DRC.
General Makenga, alisema kwamba pamoja na mapito ya kupigana, bado ana imani watu wanaweza kuweka nguvu pamoja na kufika wanakotaka.
Ziara yake hiyo iliambatana na kupelekewa msaada wa chakula, kwa kuwa wana imani dawa bila chakula hazina msaada kivile.