Gen Z Kenya na mkutano na rais

Gen Z Kenya na mkutano na rais

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Nimeona watu wakijenga hoja kwamba “huyu kijana ameongea vizuri BILA MATUSI, KEJELI, WALA LUGHA YA KUUDHI” na kwa namna fulani wanawanyooshea kidole wale wanaotumia “LUGHA KALI” kuwasilisha malalamiko yao Tanzania.

Kwanza niseme ni privilege ya hali ya juu kuwa na nafasi ya kusikia UKALI WA LUGHA katikati ya malalamiko ya tabu na mateso wanayoyatoa watanzania walio wengi.

Inaonesha tupo obsessed sana na matumizi ya lugha badala ya uhalisia wa yanayosemwa kanakwamba lugha ni muhimu kuliko maumivu ya watu.

Lakini pia silaumu sana hii obsession ya matumizi ya lugha kwa sababu kwa namna moja au nyingine ni strategy ya kuyaondolea uhalali malalamiko ya watu.

Hata hivyo kwa sababu tumeamua kuipa lugha uzito, basi ngoja tujaribu kuijadili ili tuone ni kwa nini watu wanaongea wanavyoongea.

Ipo hivi, matumizi ya lugha sio jambo geni kwenye siasa, wataalam wa sayansi ya jamii kama Mfaransa Pierre Bourdieu wanayaita SYMBOLIC CAPITAL.

Kwa lugha nyepesi, namna unavyotumia lugha ni matokeo ya matumizi ya lugha yaliyokuzunguka kipindi chote wakati unakua mpaka umefika hapa.

Kwa sababu tunajifunza lugha na matumizi yake kupitia social exposure, jinsi mtu anavyoongea ni matokeo ya hiyo exposure.

Mfano mzuri wa hili tunaweza kuuona kwa kuangalia matumizi ya lugha ya watu wawili maarufu kwenye historia; MARTIN LUTHER JR na MALCOM X.

Mara nyingi Malcolm amekuwa akikosolewa kwa hoja kwamba yupo TOO RADICAL kutokana na ukali wa lugha yake na kwamba Luther ni “bora zaidi” kwa sababu “anatumia lugha vizuri, anajenga hoja bila lugha ya kukera.”

Lakini ukijaribu kufuatilia makuzi ya hawa wawili, Malcom akiwa kijana wa mtaani aliyespend sehemu kubwa ya maisha yake katika harakati za watu wa tabaka la chini kabisa akifanya shughuli kama vile kuuza madawa ya kulevya, kamari, kukuadi “makahaba” na hata kupelekwa magereza, ni dhahiri kwamba matumizi yake ya lugha yataakisi ukuaji huo.

Hii ni tofauti na Luther ambaye kwa kipimo cha watu wa hali ya chini ni tunaweza kusema amekulia kwenye mazingira ambayo ni semi-royal.

Mazingira ya familia yenye wasomi, wenye uwezo fulani wa kipato, na lakini pia wenye elimu ya dini.

Haya ni mazingira yaliyompa Luther nafasi sio tu ya kupata elimu bora bali pia kujamiiana na watu wanaotumia lugha tofauti na aina ya watu waliozunguka maisha ya Malcolm X.

Kwa hiyo kumshetanisha Malcolm kutokana na matumizi yake ya lugha huku ukimtumia Luther kama yardstick ni sawa na kumhukumu mtu kwa kosa la kukulia kwenye tabaka fulani.

Lakini kuna jingine la msingi, maumivu ya maisha aliyoyapitia Malcolm yanamfanya azungumze kwa uchungu na hasira zaidi kuliko Luther.

Japo wote walikuwa watu weusi na kwamba walikuwa subjected kwenye systemic racism with its discriminatory practices, Malcolm, kwa nature ya maisha yake, alikuwa mhanga wa mfumo huu zaidi kuliko Luther.

Kutokana na maisha yake ya street hustling, Malcolm alikuwa anazungumza kwa maumivu na hasira kubwa kwa sababu alikuwa anayaongea maisha aliyoyaishi moja kwa moja.

Hii ni tofauti na Luther ambaye kwa namna fulani alikuwa anazungumza kuhusu maisha ya watu wake wengi ambayo yeye mwenyewe alikuwa, kwa kiasi fulani, hayaishi moja kwa moja.

Kwa mfano, kuna tofauti kubwa katika matumizi ya lugha kwa mtu ambaye analalamika mtoto wake kuuawa na polisi na mtu mwingine ambaye anamzungumzia mtu ambaye mtoto wake ameuawa na polisi.

Uchaguzi wa maneno kwa hawa watu wawili pamoja na hisia zilizopo kwenye uwasilishaji ni lazima vitakuwa tofauti.

Hoja yangu ya msingi ni hii, kila mmoja wetu anatumia lugha kwa namna inayoakisi ama makuzi yake au namna anavyoguswa na anachokiongelea au vyote kwa pamoja.

Kama ambavyo huwa ninasema mara kwa mara, mtu aliyekanyagwa ana haki ya kulia kutokana na namna anavyohisi maumivu na kwa kuzingatia kile anachotaka kufanywa na aliyemkanyaga.

Kama asingekanyagwa asingelia na kama asingelia kusingekuwa na haja ya kuchambua namna anavyolia.

Attention yetu inatakiwa kuwa kwenye kukanyagwa kwake badala ya namna anavyolia.


View: https://x.com/EduTalkTz/status/1828086913598701910?t=6Pjk89-UnI512z5F9xw7bw&s=09

Credit: Onesmo Mushi X
 
Back
Top Bottom