Ndugu wadau wa elimu, nimekuwa nikifikiria namna ya kusaidiana kupanua wigo wa uelewa wetu kupitia 'general questions' au quiz. Nadhani mtapenda kama ninavyopenda.
Nawaalika wote wenye maswali au mambo ambayo tunaweza kushirikishana kupanua uelewa wetu tuyaweke hapa. Nashauri kama mtu akiuliza swali na kama halitapata jibu haraka, basi yule aliyeuliza hilo swali atoe jibu mwenyewe ili kurahisha kujifunza kwetu. Leo naomba mimi nitoe 'quiz' yangu. Nashauri tuchangie kwa Kiingereza au Kiswahili.
Quiz yangu ya leo ni hii: Ni nchi gani duniani yenye bendera yenye rangi moja tu? Ni rangi gani na nchi hiyo iko bara gani?