General Moses Phiri na rekodi za kuogofya!

General Moses Phiri na rekodi za kuogofya!

ninosi

Senior Member
Joined
Jun 30, 2022
Posts
151
Reaction score
333
Tukiwa tunaelekea 23/10 "Wazee wa Historia" A.K.A Mabingwa wa Kihistoria naomba niwajuze historia hii!

Moses Phiri ambaye nchini Zambia hutambulika kama "Moses of Our Time" na akiwa Tanzania kama "General", rekodi zake katika vitabu vya "Historia" zinaogofya mno! Kwanini nasema hivyo, ungana nami.

Msimu wa 2019/20 wakati akiitumikia timu bora ya Zanaco katika ligi ngumu sana ya Zambia alifunga mabao 14 akishika nafasi ya pili nyuma ya mfungaji Bora wa msimu, James Chamananga aliyemaliza na mabao 16.

Jambo hili lilimuumiza sana, ambapo msimu uliofata (2020/21) aliitikisa vilivyo ligi ngumu sana ya Zambia, na hadi msimu unaisha alikua mfungaji bora akitupia mabao 17 huku James Chamanga akimaliza na mabao 11 tu. Msimu huu sasa jina "Moses of Our Time" ndiyo lilikua likitajwa kila kona.

Katika msimu wa 2021/22 "Moses of Our Time" katua katika moja ya timu bora kabisa katika bara la Africa, Simba SC. Moto wake wa kupachika magoli umeongezeka maradufu, na hadi msimu unaisha sidhani kama kuna rekodi itabaki salama.

Ukiangalia rekodi zake mpaka sasa, nawashuri TFF waandae viatu viwili vya wafungaji bora, kimoja wampatie kabisa "Moses of Our Time" na hiko kingine ndiyo waachiwe kina Lusajo, Mpole na Makambo wakigombanie.

NB: 23/10 TFF karibuni Mkapa Stadium mshuhudie kwanini nashauri msimuweke ligi moja "Moses of Our Time" na kina Lusajo na wenzake.
 
Mkuu fanya mazoezi,kula vizuri na malizia na maji kwa wingi...hakika usingizi utaupata
 
Kuelekea mazoezi ya Simba SC kwa ajili ya Group Stage za CAFCL mnamo 23/10 .. 'Moses of Our Time' kazungumza haya...

"Kwenye ligi nimefunga mabao manne naamini huku ninayo nafasi ya kuongeza idadi ya mabao kutokana na wakati huu napata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwa hiyo sitaki kuliangusha benchi la ufundi linaloniamini."

ANGALIZO: Ukiangalia rekodi za 'Moses of Our Time' katika misimu 2 iliyopita kwa kutumia elimu ya 'CUBA' nawashauri ndugu zangu.. Chonde Chonde 23/10 msilete timu uwanjani.
 
Back
Top Bottom