Kwa mara na namna ya pekee kampuni hili kubwa sana hapa Marekani na duniani la General Motors (GM) limekiri kufulia. Katika ulimwengu wa kwanza na dunia kwa ujumla kampuni hili ambalo ni taswira ya Marekani duniani katika nyanja ya utengezaji na uundaji wa magari mfano chevrolets, hammer, nk. pamoja na kuwa na mfano mzuri wa kuigwa katika uongozi na hata kuwa katika mada za kujifunza uongozi katika kada mbalimbali za elimu ya uongozi na usimamizi wa mashirika duniani. Jinsi pia serikali ilivyoingilia kati kupasi kampuni hili baada ya kufulia ni jambo ambalo nchi yetu yapaswa kusoma au kujifunza jambo. Serikali haikuridhia kampuni kubinafsishwa au kuuzwa kwa makaburu kama sisi tungeweza kufikiri ndio suluhu ya mwisho. Je, GM na mashirika yetu nyumbani yaliyofulia, tunajifunza nini? Je yalifulia kwa mtindo huo wa GM? Nini cha kufanywa na serikali yetu kama somo kutoka kwa GM kwa viwanda na makampuni yetu yaliyofulia ukiachana na hali ya uchumi kwa ujumla?