Generation Mwinyi katika CHADEMA VS Chairman Mbowe

Generation Mwinyi katika CHADEMA VS Chairman Mbowe

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Natoa uzoefu kwa mambo nayoyakumbuka katika siasa za upinzani tangu nikiwa sekondari. Soma mpaka mwisho maana suala la Mbowe lipo mwisho mwisho.

Binafsi nimezaliwa enzi za Mwinyi. Hii generation ndio ambayo ilitarajiwa kukuza upinzani katika siasa za mfumo wa vyama vingi kwa sababu mbalimbali.

Hii ni generation ambayo tulipoanza kujitambua kiakili mwishoni mwa miaka ya tisini kuelekea miaka ya 2000 ndipo CHADEMA ilikuwa inafanya harakati za kukikuza chama. Hivyo Gen Mwinyi ilikuta CHADEMA wapo hot na zile helkopta zao katika kampeni mbalimbali.

Nakumbuka katika uchaguzi wa 2005 tulikuwa tunaenda kumshangaa Mbowe alipokuja na helkopta katika kampeni za urais.

Haters walimponda Mbowe kuwa kampeni zake zinafuatiliwa na watoto. Ni kweli, watoto wengi kipindi hicho tulienda kushangaa helkopta.

Lakini miaka kumi baadae kuanzia 2010 -2015, wale watoto waliokuwa wanashangaa helkopta, hao ndio wakawa followera wakubwa wa CHADEMA kwa sababu ndio walikua wakiona harakati zao, ikizangatiwa waliona harakati wakiwa watoto hivyo kukaa kichwani.

Kuanzia 2010 CHADEMA ilikuwa na base kubwa ya followers vijana wale waliozaliwa enzi za Mwinyi. CCM walijisahau kidogo kutowekeza kwa vijana wa Gen Mwinyi kwa kipindi hicho.

Kama mnakumbuka miaka 2010 baada ya migomo mingi vyuo vikuu, serikali ilipiga marufuku siasa vyuoni kwa sababu vijana wengi walikuwa wapinzani.

Katika uchaguzi wa 2010 kama mnakumbuka, vijana mawakala wa upinzani walikuwa tayari kulinda kura bure kabisa bila hata kula siku nzima huku mawakala wa CCM wakiletewa msosi wa maana. Leo kila kijana kwenye siasa anatafuta hela, hivyo muda wowote anaweza kununulika na hawaaminiki tena.

Kwa mfano, kipindi cha 2010, vijana wa upinzani vyuoni wa Gen Mwinyi waliahidiwa teuzi lakini walikataa na hata huko CHADEMA siyo kwamba walikuwa wanapewa hela, ni basi tu roho ya harakati ilikuwa damuni mwao.

Mambo yalikuja kuharibika kuanzia 2015 ambapo kupigwa pini kulipelekea uchawa ambapo vijana wakalainika na kuanza kuunga mkono juhudi.

Kwa upande wa Gen Z ya Tanzania ni kama vile haina mwelekeo wowote na siasa za nchi hii. Sijajua kama wanajitambua au ni mazingira ndio yamewafanya hivyo kuanzia mfumo wa elimu nk.

Kuanzia 2005 na mpaka sasa, Gen Mwinyi imeshuhudia harakati mbalimbali za CHADEMA chini ya Mbowe mfano M4C, Operation Sangara nk.

KUHUSU MBOWE KAMA MWENYEKITI

Hakika, ukiwauliza followers wa CHADEMA kutoka Gen Mwinyi watakwambia inatosha kwa Mbowe kuwa mwanachama.

Mabadiliko hayazuiliki. Huko nyuma sijui Mbowe alikuwa ana kismati gani kwa sababu alikuwa anaongezewa muda na wanachama walikuwa wanakubali tu, lakini leo hii kiukweli Mbowe kachokwa.

Umaarufu na uhai wa CHADEMA umeshikiliwa na Mbowe mpaka sasa. Hii ina maana kuwa, Mbowe akiwa mwenyekiti hawezi kuja kuwaeleza wanachama sera na hoja mbalimbali wakamuelewa mana ameishachuja. Mbona Biden alipoona amechuja akajiongeza tu, iweje Mbowe!

Lisu naye ni hatari sana kwa tabaka tawala mana jamaa hana subra kabisa. Anaweza kuanzisha maandamano hata peke yake. Hii ni hatari kwa sababu nature ya vijana ni kupenda heka heka, hivyo Lisu anaweza kupata wafuasi vijana wengi na wakamuunga mkono hasa akipitia suala la ajira na ugumu wa maisha.

Kwa upande mwingine, Lisu anaweza kuwa na faida kwa kuimarisha upinzani ambapo upinzania ukiwa hai, hata serikali nayo inakuwa active katika kutatua changamoto za wananchi.
 
Generation Mwinyi ndio Generation ya machawa.
Inasikitisha sana kwa sababu hii generation ndio iliukuza upinzani lakini kwa sasa ndio machawa baada ya kubadilishwa na siasa za Jiwe.

Gen Z haina hata wazo na siasa, yenyewe ipo bize na mziki na viduku.
 
Inasikitisha sana kwa sababu hii generation ndio iliukuza upinzani lakini kwa sasa ndio machawa baada ya kubadilishwa na siasa za Jiwe.

Gen Z haina hata wazo na siasa, yenyewe ipo bize na mziki na viduku.
GenZ ya TZ ipo busy na amapiano +singeli.
Outraged.
 
Back
Top Bottom