PostGE2025 Genge la Abdul linamuona Nchimbi kama tishio

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Umeimalizia kibabe dah!🤣
 
 
Kwa hali hii huenda wakarekebisha hicho kipengere cha sheria bungeni kuzuia makamu wa Rais kuwa Rais endapo Rais anakuwa katangulia mbele ya haki, wanajua ikiwa Nchimbi anakuwa Rais watafungwa jela wote na kufisiwa mali zao walizopora na kuficha popote Duniani
 
Sasa Nchi ipo njia panda badala ya kupoza machungu wanaongeza hasira kwa wapenda haki kwa kuwabambikia Heche kesi ya Uongo huku wakipanga njama za kumtoa Nchimbi kwenye umakamu wa Rais, hicho kikundi kimejaa ushetani wa kutisha ni vyema wasomewe Albadiri mapema kabla hawajaenda mbali
 
Hapo kwenye kubadili kipengele cha makamu wa Rais kuja kuwa Rais ikiwa kitatokea chochote kisichotarajiwa nasikia nikweli , huu mjadala upo active sana hata sasa kwenye kamati nyingi za ulinzi na usalama .

Ila hapo kwa Nchimbi kuja kuwa bora na pengine kuja kuwageuka kindi lililompambania kumuweka alipo ,nadhani ninamna tu yakujitengenezea faraja ya bandia

Chakwanza licha tu ya Nchimbi kutokuwa na hiyo spirit lakini muundo wa hayo kuja kufanikiwa siyo mwepesi kwa kiwango hicho wazee .

Kundi la mtandao ni moja kati ya makundi hatari sana Duniani , kabla hawajaridhia kumuweka kwenye hiyo nafasi ,jamaa alipembuliwa kwa viwango vyakutosha sana na mwisho akaonekana hana madhara kwao
 
Nchi imejeruhiwa sana yafaa itibiwe kwa kufanya maridhiano na walioathirika sana ilibidi walipwe fidia kuombwa msamaha, Serikali ya ccm iache kuzidisha chuki kwa kuendelea kamata kamata watu hovyo kuwabambikia kesi za uongo , Serikali ya kupenda kesi kesi ni serikali ya hovyo kwani hakuna binadamu atawapenda viongozi watesi waonevu wanaotumia mda mwingi kuonea watu badala ya kuleta maendeleo
 
💯%
 
Nchi inahitaji faraja Nchi haihitaji kesi kesi kamata kamata kesi kila kata wilaya mkoa kwani kwenye huo mfumo waonevu hutumia fursa kuwaonea watu kuwatengenea kesi wapate Rushwa pia kuwakomoa kwa chuki binafsi, Tanzania ya sasa inahitaji maombi maalumu kuwarejesha watanzania pamoja siyo kuwatesa kwa kutumia polisiccm na mahakamaccm
 
Watavurugana tuu kati yao, wamemwaga damu nyingi sana zisizo na hatia, ila sisi hatusubiri hilo kupata mabadiliko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…