Geoffrey Lea rasmi EFm katoka Clouds Fm

Industry inazidi kunoga na kuchangamka,hata guyo Geof husi shangae akarudi CMG hii biashara kila mtu anatizama maslahi yake.
 
Huyu inabidi atulie sehemu moja ajenge career yake hata kama maslahi ndio kigezo, utafika wakati atakosa pakwenda, akumbuke hiyo ni mikataba tu na ina ukomo wake
Alikuwa CMG, Akaenda AZAM, Shafii akamrudisha CMG, Sasa kasepa EFM, Baadae tutamuona WASAFI FM
Kila la heri baada ya msiba wa mama yake hajawa sawa jamaa basi tu
 
Mwenye data atujuze, nini kilichomkimbiza Jeof Lea pale Azam TV? Mahali ambapo kila mtangazaji anatamani awepo kutokana na mishahara yao minono?
 
mayowela we Ni mdau mkuu Sana wa Media kiujumla naomba nikuulize unaionaje kipindi kipya Cha Wasafi tv Cha Big Sunday live?kuhusu huyo jamaa Jeff Lea sijawahi kumkubali kabisa kwa sababu una ushabiki wa man United katika uchambuzi wake ajui kuleta balance kwenye uchambuzi.
 
Mwenye data atujuze, nini kilichomkimbiza Jeof Lea pale Azam TV? Mahali ambapo kila mtangazaji anatamani awepo kutokana na mishahara yao minono?
Percy Kama ingekuwa Azam wanalipa mishahara minono Ahmed abdallah asingehama na kujiunga na Wasafi media labda uniambie wanalipa mishahara minono kwa baadhi ya Wafanyakazi nitakuelewa.
 
Big Sunday Live ni kipindi kizuri, kimeenda na wakati na content ambazo wengi wanafanya kama Clouds+ na the Giant, ETV na HOMA, Clouds tv na Washa Kideo, sikuhizi hakuna clubs so watu ambao sio wa mitoko wamewateka, ila tu, wangepunguza watangazaji angalau wabaki wawili
 
Jamaa yuko vizuri ila mambo yake ya kuvaa hereni ndo yanaboa
 
Percy Kama ingekuwa Azam wanalipa mishahara minono Ahmed abdallah asingehama na kujiunga na Wasafi media labda uniambie wanalipa mishahara minono kwa baadhi ya Wafanyakazi nitakuelewa.
Kuna wakati mtu anahama sehemu sio tu maslahi, pia uhuru wa kazi na kupewa nafasi, kuna watu wako sehemu kubwa ila hawako huru kufanya kazi, hawapewi nafasi ya kusikika hawana maamuzi, haya mambo hupelekea mtu kuondoka hata kama dau limeongezeka laki
 
Huyu Jeff bhana kila siku anahama hama alikuwepo azam,clouds mara saiz tena efm. Lakini yote maisha.
 
Clouds ruge alikuwa anaibeba sana.

Kusaga haitendei haki clouds , nguvu kubwa kaiwekea wasafi media..

Yaani tajiri wenu ana kampuni mbili zinazoshindana.. halafu moja anaiwekea nguvu kubwa , lazima wafanyakazi mjisikie vibaya...msepe
Wasafi kua pale sio investment ya kusaga..wasafi ni brand tu ndio iliyowasimamisha.....yani kweny brand kusaga hatingishi hata kiberiti...na ukiwa na brand hata uje na billions of money haufui dafu...Kwnini wagumu kumuappreciate Almasi?
 
mayowela Katika vipindi hivyo vyote kipi kwako unaona ni Bora kuliko vyote na panga kwa mpangilio kuanzia moja mpaka ya mwisho
 
Baada wiki iliyopita kumchukua moja watangazaji giant wa clouds (B DOZEN) leo EFM wamemtangaza pia kumchukua GEOF LEA mchambuzi wa Michezo hii inaonesha jinsi gani EFM wanajipanga kuwa moja kati ya radio station kubwa tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…