Geor Davie ni nani?

Kha!! Ngoja nijaribu kuufufua huu uzi! Na mimi naweza kuitwa nabii eti!! Ila huyo mnyeramba anaonekana mpigaji aisee, Nabii mjanja mjanja!!hahahaaa
Sioni tena misafara yake siku hizi,bado yupo kwenye game?
 
Ha ha ha ha haha 😂 hivi mnaamini kweli kuwa hawa ni manabii, mi naona ni wapiga dili kama walivyo ....
 
Mi nikisikiaga nabii au mtume tu taa ya tahadhari inaanza kuwaka.
 
Hakuna kinachowasukuma zaidi ya pesa. Na watu sijui nani aliyewaloga. Wanafuata hawa manabii so blindly kama kondoo anayeongozwa kwenda machinjoni
 
Huwa nasikiliza redio zao usiku na kubaki nacheka tu. Wanataka pesa tu. Utaambiwa kabla ya kupeleka maombi yako kwa Mungu kamata Pesa (sadaka) yako mkononi kwanza iombewe!!
 
Huwa nasikiliza redio zao usiku na kubaki nacheka tu. Wanataka pesa tu. Utaambiwa kabla ya kupeleka maombi yako kwa Mungu kamata Pesa (sadaka) yako mkononi kwanza iombewe!!
Waumini nao wala hakuna anayejiuliza kama jambo hili linaendana na mafundisho ya Biblia juu ya maombi.
 
Waumini wengi wanaokwenda kwa hawa manabii na mitume wanakwenda huko kwa tumaini la kutatuliwa matatizo ya maisha tu na si kutafuta kumjua Mungu. Jambo hili Yesu alilikemea baada ya kuwalisha kundi la watu kwa mikate wakashiba wakasaza, ikawa kesho yake wakawa wanamtafuta for the same reason! Si kwa sababu walitaka tena kusikia mafundisho yake bali walitaka tena kujaza matumbo yao.
 
Kama wewe ni mkristo sahihi unatakiwa kujua kuwa Yesu alipokufa pazia la hekalu (lile ambalo Kuhani mkuu pekee aliruhusiwa kuingia pale kwenye uwepo wa Mungu) lilipasuka hivyo kila mwamini wa kweli anajua anayo tiketi ya kumwendea Mungu bila kupitia kwa hao ambao sasa naona nia yao ni kulishona tena lile pazia lililokwisha kupasuliwa na kututaka tuwape pesa ili wao waingie kule nyuma ya pazia ati watupelekee maombi yetu!!!
 
Mkuu si umtaje tu...si ni Weston yule aliekuwa hoopoe adventure.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo Uzi wa siku nyingi Ila Nina hakika wewe utakua kichaa
 
wewe akili huna tema pole sana kwa hili
 
Habarini za nyakati hizi wapendwa,

nimepata wasaa wa kufuatilia baadhi ya video za chaneli ya YouTube yake na nimekuwa nikiona akitoa hela kwa wasanii, waandishi wa habari mpaka magari.

Je, kuna injili ya kweli hapo au? Wanaomfahamu tafadhali taarifa zaidi tunaomba.
 
Inawezekana ikawepo. Kwani hujui kua injili ni biashara siku hizi
 
Hakuna watu wenye vichwa vibovu kama walokole. NA ZAMA HIZI NI KAMA VICHAA . MWENYE AFYA YA KILI HUWEZI FUATISHA HAO WATU!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…