Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
GEORGE ARNAUTOGLU
Ukumbi wa Arnautoglu ulikuwa ukumbi maarufu sana Dar es Salaam katika miaka ya 1950 na shughuli nyingi za kijamii na za kiasi zimefanyika pale.
Jambo la kusikitisha sana ni kuwa hakuna mtu amjuaye mjenzi wa jengo hilo wala hakuna picha yake popote katika hilo jengo.
Wala historia ya George Arnautoglu haijulikani sana na wanoijua watakuambia kuwa alikuwa Giriki tajiri mwenye mashamba ya mkonge.
Hapo chini ni picha ya George Arnautoglu niliyoletewa na Hafidh Kido mwandishi wa Jamvi la Habari kutoka gazeti la Mambo Leo la mwaka wa 1943.
Nimekutana na George Arnautoglu wakati natafiti historia ya TANU siku nilipokwenda kuzungumza na Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mmoja wa viongozi wa juu wa TANU katika siku zake za mwanzo miaka ya 1950
Ali Mwinyi Tambwe anasema aliwahi kupewa fedha nyingi na George Arnautoglu azifikishe TANU zisaidie harakati za uhuru.
Ali Mwinyi Tambwe alinieleza kuwa George Arnautiglu akiwachukia sana Waingereza kwa kuwa wakati ule Ugiriki ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza na wananchi walikuwa wanapambana na ukoloni huu.
Hii ikawa sababu kubwa ya George Arnautoglu, Mgiriki kuwachukia Waingereza.
George Arnautoglu kwa kuonyesha shukurani kwa Tanganyika nchi ambayo ndimo alimotajirika aliwajengea watu wa Tanganyika Ukumbi wa Arnautoglu kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya Waafrika.
Picha ya pili ni Ukumbi wa Arnautoglu.]