George Job: Simba haiwezi mechi za mtoano

George Job: Simba haiwezi mechi za mtoano

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Mchambuzi wa michezo kutoka Wasafi Fm, George Job amesema klabu ya Simba bado haijajiandaa vema katika mechi za mtoano.

Kikosi cha Simba ilkinaweza kupambana vizuri kwenye mechi za makundi ila linapokuja suala la mechi mbili za mtoano hapo ndipo ulipo mtihani kwa Simba SC.

Kwa kauli hiyo ni wazi George Job anaona kabisa kuwa Simba inaenda kutolewa na Orlando Pirates.

DAD1B54A-FE4E-4B7C-BD75-B22C2EA7EBB5.jpeg

1426B56A-9040-470F-A18F-BE6562DCAA6B.jpeg
 
Kuna kaukweli katika hili, sababu mara zoote tumetolewa kwenye hatu hii tuliyofika, tuache muda uzungumze japo simba ya msimu huu sina matumaini nayo makubwa, last season tulizinguwa kwa wale Kaisari wa kwa madiba, ulikuwa msimu wetu ule kufika mbali.

Tukishinda zaidi ya goli 3 kavu hapa home kuna nafasi kubwa kutoboa ila sioni kama inawezekana.

Tuombe mungu
 
Wachambuzi ni wengi sana mpaka atuwaelewi, kwani hatua ya makundi sio hatua ya mtoano?,ni mtoano wenye mzunguko wa mechi sita home & away.

hatua iliyopo Simba ni hatua nyepesi kwa timu yeyote kuliko hatua iliyopita.
 
ILA hawa jamaa naona wañacheza aloo .....hawakati tamaa hata wakiwa ugenini. Nimejaribu kuwafatilia mechi walizocheza karibuni .....
Udhaifu wao pia n setpieces na mipira ya Kona.
 
Mmezidi kuwa attack wachambuzi cha ajabu bado mnafuatilia vipindi vyao, mimi pia ni shabiki wa Simba lakini nakubaliana na George Job!

Kama msimu uliopita hadi leo najiuliza Gomes alifikiria nini kwenda kushambulia ile game ya ugenini!.

Hata hii game sina matumaini sana maana kocha ana team selection mbovu sana, sitashangaa akianza na Kibu akamuacha BM 3 au Banda nje!.
 
Hii kiasi fulani naona kama ina ka ukweli fulani hivi, ngoja tupambane kuyashinda haya!
 
Simba kwenye groups ingekuwa mtoani angeitoa timu moja tu hii Niger usgn ambayo kule sare 1- 1 na Dsm Simba kashinda 4-0.
Yeye na Asec Dar 3-1, kule kapigwa 3-0 na zingekuwa zaidi kama sio Manula, na Berkane kule Morocco 2-0 kafungwa hapa kashinda 1-0.
Kwa hiyo kwa mtoano ana asilimia chsche sana kupita na hassa huko kuna kuwa na timu zenye uwezo mkubwa zaidi.
Bahati ns fursa pekee ya kuweka historia ilikuwa na kaizer Chiefs (ambayo ilikuwa dhaifu) ilipofungwa 4-0 na simba kushinda 3-0 katika mechi ambayo ya hapa walikuwa na uwezo wa kushinda hata 5-0.
Kwa mechi ya jumapili lazima washinde 3-0 la sivyo watatolewa na hassa ukizingatia Orlando Pirates wapo vizuri saana, na Simba wapo chini kuliko msimu uliopita japo miujiza kwenye soka yapo.
Na kwa Simba hii hapa walipo fika wamefanya vizuri sana , maana timu bado haipo vizuri.

Illa ikijengwa vyema na hassa kwa viongozi kuwa na uzoefu wa mashindano ya kimataifa Simba huenda siku moja itafanya maajabu lakini lazima usajili uwe bora angalau wachezaji wanne wa nje na wanne ndani ambao wapo over average.
Ni hayo tu.
 
Mchambuzi wa michezo kutoka Wasafi Fm, George Job amesema klabu ya Simba bado haijajiandaa vema katika mechi za mtoano.

Kikosi cha Simba ilkinaweza kupambana vizuri kwenye mechi za makundi ila linapokuja suala la mechi mbili za mtoano hapo ndipo ulipo mtihani kwa Simba SC.

Kwa kauli hiyo ni wazi George Job anaona kabisa kuwa Simba inaenda kutolewa na Orlando Pirates.

View attachment 2186055

View attachment 2186056
HUENDA YUKO SAWA

ANYWAYS, NGOJA NITUNZE COMMENTS ZANGU, Baadae nitarudi kufufua hili kaburi
 
Kwa mara ya kwanza nakubaliana na huyu mshabiki wa mpira, ni kweli Simba haijajipanga kuvuka robo maana matatizo ya timu ni yale yale kila msimu.Hii hatua tuliyofika ni bahati tu.
Mchambuzi wa michezo kutoka Wasafi Fm, George Job amesema klabu ya Simba bado haijajiandaa vema katika mechi za mtoano.

Kikosi cha Simba ilkinaweza kupambana vizuri kwenye mechi za makundi ila linapokuja suala la mechi mbili za mtoano hapo ndipo ulipo mtihani kwa Simba SC.

Kwa kauli hiyo ni wazi George Job anaona kabisa kuwa Simba inaenda kutolewa na Orlando Pirates.

View attachment 2186055

View attachment 2186056
 
Ukiondoa ushabiki george job amesema kweli timu ya msimu huu tia maji away msimu uliopita ndio ulikua mzuri sana …Kocha wetu huyu anabebwa na wachezaji pale hamna kocha msimu ujao kufika mbali tunahitaji kocha anaeeleweka yeye kila siku kulalamika viwanja hana plan B ?
 
Back
Top Bottom