Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
GEORGE WASHIGTON RAIS WA KWANZA WA MAREKANI MZALENDO NA MTAIFA AMBAYE FALSAFA ZAKE ZILIITENGENEZA MAREKANI KUWA TAIFA IMARA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu
Sartuday -16th/12/2017.
Nilidhamiria kuandika makala hii katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya Washigton Day (iliyoadhimishwa siku ya juzi ya tarehe 14/12/2017 huko marekani) ambayo husherekewa kila siku ya tarehe 14 ya mwezi wa 12 ya kila mwaka nchini marekani lakini kutokana na afya yangu kutokuimalika vyema nilishindwa kuikamilisha kwa wakati. Hivyo niliona vyema kuikamilisha ili kutimiza ombi la rafiki yangu Hamdani Mbwana aliyepata bahati yakuwa mgeni katika kumbukizi hiyo katika ubarozi wa Marekani nchi Tanzania kama afisa utamaduni wa ndani.
Kufatia maombi yake nikaona vyema kuandaa makala hii angalau kwa uchache ili tuweze kumfahamu Washington kwa uchache wake. Kutokana na umuhimu wa Washington katika siasa za marekani ikumbukwe kuwa yeye ndio mwanzilishi wa wazo la kuunda taifa lenye mfumo wa shilikisho na yeye ndie alipendekeza kuunganishwa makoloni 13 ya awali na liundwe taifa moja mara baada ya kumalizika kwa vita ya ukombozi mwaka 1788 niyeye aliyependekeza jina linalotumika sasa la “umoja wa mataifa ya marekani” (United State of America) na niyeye aliyependekeza wazo la mfumo wa kuwapata viongozi wao wa taifa hilo mfumo ujulikanao kama “Mfumo wa Chaguzi kwa kongamano” ( Electro College).
Ikumbukwe George Washington aliongoza kikosi cha wanamgambo kwenye vita ya ukombozi na baadae kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa balaza la kuunda katiba (Constitution Convetion) huko Philadephia kwenye kongamano la katiba na yeye ndie muasisi wa utaratibu wa kupokezana vijiti katika utawala nchini marekani. Moja ya taratibu alizozipendekeza ndizo zinazoendelea kutumika nchini marekani mpaka leo na kuifanya katiba ya marekeni kuwa moja ya katiba bora dunia hadi sasa.
George Washington alizaliwa tarehe 22 Februari 1732 hadi tarehe 14 Desemba 1799 alipofaliki dunia nyumbani kwake huko Mount Vernon Virginia alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797 washington pia hutambulika kama baba wa taifa wa marekani pia ni miongoni mwa wasisi wa taifa hilo kati ya wasisi 22 wanaotajwa kwenye Agano la uhuru (independence Declaration) katika taifa hilo kubwa kiuchumi na linalotajwa kukomaa kisiasa.
Washingoton alizaliwa kama mtoto wa pili wa mlowezi Augustine Washington katika koloni ya Virginia iliyokuwa mali ya mfalme wa Uingereza (lakini alikuwa ni mtoto wa kwanza wa Augustine Washington kwa mama yake Mary Ball Washington ambaye alikuwa ni mke wa pili wa Augustine Washington ) . Wazazi walikuwa na mashamba makubwa ya tumbaku lilolimwa na watumwa Waafrika. George alisoma shule miaka michache hakuendelea sana kielimu. Baada ya shule alianza kazi ya upimaji wa ramani (surveyor).
Baada ya kifo cha kaka yake mdogo alirithi shamba kubwa lilokuwa mali ya kaka yake pamoja na watumwa akawa mkulima tajiri huko Virginia. Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimazi wa wanamgambo pia waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi wa Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio (red indies) na Wafaransa katika vita ya (french Indian War) walioenea katika maeneo ya kusini kutoka koloni yao ya Kanada - Quebec.
Ikumbukwe kuwa wakati huo Uingereza ilitaka kuyapokonya makoloni ya ufaransa ya Amerika ya kaskazini ambapo yalikuwa chini ya ufaransa (Canada ya leo) na jambo hili ndilo lilichochea chuki kwa wafaransa na kusababisha kuchochea hali ya ufaransa kuja kuwasaidia askali wa makoloni 13 ya marekani yalipokuja kudai uhuru kama sehemu ya kulipiza kisasi.
Akiwa Katika umri mdogo wa miaka 22 Washington alijikuta kama mkuu wa wanamgambo katika vita ya Uingereza dhidi ya Wafaransa na Waindio iliyopanuka baadae kuwa Vita ya Miaka Saba (7 years war). Baadae akaongoza kikosi chake dhidi ya maadui akafaulu mara kadhaa. Baadaye alishirikiana na jeshi rasmi la Uingereza katika mapigano ya Monongahela na kuongoza mabaki ya jeshi baada ya kifo cha jemedari wa kingereza. Mwaka 1755 akawa mkuu wa jeshi la koloni Virginia.
Lakini baada ya ushindi Waingereza walikataa kumpa cheo katika jeshi la mfalme hivyo akajiuzulu na kuamua kurudi zake kwenye shamba lake na kuamua kuanza kujishughulisha na siasa kwenye bunge la koloni. Hata hivyo mwaka 1759 Washington akavunja ukapera akamwoa mjane tajiri aliyeitwa Martha Dandridge Custis akawa kati ya matajiri wakubwa kabisa wa jimbo la Virginia.
Baada ya vita ya miaka saba uhusiano kati ya Uingereza na walowezi Waingereza katika koloni zake 13 za Amerika ya Kaskazini ukazorota sana. Tangu 1773 Waingereza walitumia sheria ya dharura na nguvu ya kijeshi mjini Boston na kupelekea mauaji ya Boston (Bostoni massacre) yaliyokuja kuwa chachu ya mapinduzi na harakati za kudai uhuru katika majimbo 13 yaliyokuwa yakitawaliwa na Uingereza. Hivyo kufatia mauaji hayo Wawakilishi wa koloni zote 13 wakakutana kama bunge la Amerika Bara na Washington alikuwa miongoni mwao.
Baada ya mapigano ya kwanza kati ya wanajeshi Waingereza na wanamgambo wa walowezi bunge likaamua kuunda jeshi la pamoja la koloni zote (Continental army) na Washington akateuliwa kuwa jemadari mkuu. Aliongoza jeshi la Marekani katika vita ya uhuru wa Marekani dhidi ya Uingereza hadi mwaka 1783 waingereza walipokubali kushindwa vita na kukubali kukabidhi uhuru kwa walowezi wa kingereza.
Baada ya vita ya uhuru ya Marekani Geroge Washington akarudi shambani kwake kuendelea na shughuri zake za kulima tena lakini akachaguliwa pia kama mwakilishi wa Virginia katika bunge maalumu la katiba (kongamano la katiba) la Marekani mwaka 1787 akawa mwenyekiti wa mkutano huu uliokubali kuandaa katiba ya Marekani.
Mnamo tarehe 4 Februari 1789 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani akarudishwa tena kama raisi mwaka 1793 mpaka mwaka 1797. Baada ya kipindi chake cha pili alikataa kusimama tena kuwania uraisi na akaunda hivyo utaratibu yakwamba rais na maraii wote watakaomfuata wanaweza kurudishwa mara moja tu na hawato weza kuendelea zaidi. Utaratibu huo uliheshimika na kuenderea kutumika kwa warithi wake wote mpaka utaratibu huo wa ukomo wa uraisi wa miaka nane kwa mihura miwili ya miaka minne ulipokuja kuingizwa rasmi kwenye katiba yao mwaka 1940 katika kile kilichoitwa marekebisho ya 22 ya katiba yao (22nd amendment)
Mwaka 1797 akarudi tena kwake shambani aliposimamia kilimo kilichoendeshwa na watumwa 390 aliokuwa akimiliki. Mnamo majira ya baridi majira ya saa nne asubuhi ya siku ya jumamosi ya tarehe 14 Desemba alifariki nyumbani kwake huko Viginia kwa ugonjwa kansa ya Koo (Epiglottitis) akiwa na umri wa miaka 69 na kifo chake kilitangazwa na mwandishi wake binafsi na msemaji wake Tobias Lear. Kabla ya kuaga dunia aliamuru katika usia wake ya kwamba watumwa wake wote warudishiwe uhuru baada ya kifo chake yeye mwenyewe na mke wake. Washington hakuwahi kuwa na mtoto wa kuzaa katika maisha yake yote.
Mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na jimbo la Washington linalopatikana Maghalibi mwa marekani vimepewa majina kutokana na yeye. Pia kwa heshima yake Picha yake iko kwenye noti ya dollar moja. Ikiwa pamoja na tarehe ya kifo chake ni tarehe ya kitaifa nchini marekani.
[emoji117][emoji420]Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
[emoji768]Wako Mjoli wa Historia ya dunia na mambo ya dipromasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji767] Copy rights of this article reserved
[emoji768]written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
[emoji769]Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com.