Mtalii wa Kisiasa
Member
- May 3, 2019
- 53
- 144
GEORGE WEAH MWANASOKA BORA WA DUNIA,ULAYA NA AFRIKA 1995.
Leo 13:15pm,29/06/2019.
George Weah akitokea ligi ya Liberia,moja kwa moja hadi klabu ya Monaco,baadae kuelekea club ya Paris St Germain na kilele chake kilikuwa alipoelekea club ya Milani na kuwa Mfalme wa San Siro,huku akina del pierro wakimuona akitawazwa kuwa Mchezaji bora wa dunia wa mwaka 1995,Ulaya nao hawakuwa nyuma,wakamtangaza kuwa Mchezaji bora wa Ulaya wa mwaka 1995,huku nyumbani nasi tukasema igwee na kumtangaza Mchezaji bora wa Afrika wa Mwaka 1995.
Baada ya George Opong Weah kutangazwa kuwa Mchezaji bora wa dunia waafrika tukang'ara kwa jina la George Weah,Waafrika waliokuwa Ulaya na wengine toka Afrika wakaenda Ulaya na kujitambulisha wao ni wadogo wa George Weah kutoka Afrika ya Magharibi.Vijana wengi waliaminiwa kwa jina la George Weah na wengine kupata kazi na wengine kusajiliwa na vilabu vikubwa barani Ulaya.
Msenegali Ali Dia aliyefulia ulaya akiwa masomoni na kuamua kutafuta ada ya shule kitaa akiwa na mwanadarasa mwenzake wakaiona fursa kwa jina la George Weah Mwanasoka bora wa Dunia,Afrika na Ulaya.Ali Dia jina maarufu kabisa liliingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mchezaji mbovu kabisa kuwahi kutokea duniani baada ya kutumia fursa na kujipatia namba kwenye kikosi cha kwanza kwenye club kubwa kabisa nchini Uingereza,club ya Southampton.
Ali Dia alipangwa kuanza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Arsenal lakini bahati mbaya barafu mechi ikahairishwa na kubahatika kuingia sub kwenye mechi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Aston Villa,kwa hakika aliandika historia ya kucheza ligi ya Uingereza japo kwa wiki mbili na kutimuliwa na kulipwa juu,historia itamkumbuka kama mmoja wa waliopata kucheza kandanda nchini Uingereza kwenye club ya Southampton kwa kutumia jina la George Weah.
Ilikuwa mchana mtulivu nchini Uingereza kwenye jiji la Southampton, ikapigwa simu kwa Manager wa Southampton ikijitambulisha kama ni George Weah ikimuelekeza Manager wa Southampton kumchukua kijana binamu wa George Weah mwenye kipaji cha hali ya juu kwa jina la "Ali Dia" kwa kuwa ni ndugu yake yeye George Weah lakini pia ni mchezaji anayechipukia na mwenye kipaji sana.
Manager akaitikia Wito toka kwa "George Weah" Mfalme wa soka wa dunia katika mwaka huo wa 1995 na kumsajili Ali Dia kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Southampton iliyokuwa ligi kuu nchini Uingereza,kumbuka simu hiyo haikuwa ya ukweli toka kwa George Weah bali ni rafiki wa Ali Dia ndiye aliyepiga simu hiyo kwenda kwa manager wa Southampton.
Mambo yalikuwa hivi kwenye waya huo aliovutiwa manager wa Southampton,..."Yes,this is George Weah calling from West Africa,introducing my cousin and a very talented young player Ali Dia,please give him the number" Manager wa Southampton akafurahi kupokea simu toka kwa Mfalme wa Soka wa dunia George Weah na akatii wito na kumtafuta kumsainisha mkataba moja kwa moja.
Mechi ya kwanza Ali Dia akawepo kwenye wachezaji wa akiba,bahati ikamdondokea mchezaji akaumia na ikawa nafasi ya kumuona ndugu wa "George Weah" akisakata kandanda kama la Mfalme wa Soka George Weah,Ali Dia aliingia uwanjani kama sub ye le tissier ,akizunguka uwanja mzima kama pimbi bila kugusa mpira,it was very embarrassing to watch how he was running na baada ya dakika ishirini akaomba kutolewa maana alikuwa amechoka!kumbe mpira hajui,ha ha haaa.
Watu walishangazwa sana hasa Manager aliyemsajiri na toka saa ile kikao kilikaa kuvunja mkataba wake,Mkataba wa Ali Dia ukavunjwa akalipwa pesa nyingi akaenda kumalizia degree yake ya Utawala na mwaka 2001 akapata Shahada yake ya pili ya Umahiri yaani Master's degree.Hivi sasa ni administrator mzuri kabisa uko Uingereza wakati Mfalme wa Soka George Weah hivi sasa ni Rais wa Nchi yake ya Liberia.Ahsante George Weah kwa kutupa heshima na fursa sisi Waafrika pale ulipotawazwa kuwa Mwanasoka bora wa Dunia,Afrika na Ulaya.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.