Hao wote ni sawa, ila naomba niende nje kdg ya hao tuwaongeleao.
Okocha ndie tunaweza kusema ni mchawi wa soka, japo hakutunukiwa mataji yoyote...ila ndie aliemuweka Gaucho benchi kwa kipindi chote walipokuwa pale PSG, na manjonjo mengi ya Gaucho aliyapata toka kwa JJ-Okocha. Bara zima la Africa halijapata kuwa na aina hii ya mchezaji mwenye kufanya lolote uwanjani na kwa mazingira yoyote yale.
Katika watu walioongea ushuzi hapa JF basi wewe unaongoza na kama likitokea punguwani jingine zaidi yako ntalinasa makofi na kulifukuza.
kwanza unatakiwa ufahamu Okocha kapiga PSG kuanzia 1998-2002.
Kisha mtakatifu Gaucho wa Dinho kakipiga kuanzia 2001 mpaka 03.
So jaribu kwenda kuangalia ni mchezaji gani kati ya hao wawili kaifungia magoli mengi zaidi PSG?
Kisha rejea kuwa wakati Okocha anaondoka PSG akaenda Bolton, je unaweza kunishawishi kuamini kuwa timu kubwa zilikuwa hazimuhitaji kwa kipindi hicho?
Au timu kubwa zilikuwa hazina pesa ya kumnunua?
Au alikataa mwenyewe na kuchagua kwenda Bolton?
Kisha nakufahamisha wewe na wakurupukaji wenzio kwa kukwambia kuwa wakati Dinho anaondoka PSG alikuwa anagombewa na Man UTD na Barca.
Na yeye kwa mapenzi yake akahamia Barca ambayo ilikuwa imepotea ktk ramani ya soka ulimwenguni kwani hata Champions League yao ya mwisho kubeba ilikuwa 1992.
Ila kiumbe aliyeshushwa baada ya Kutua Catalunya akaisaidia Barca kushika nafasi ya pili ya ligi ya La Liga kwa msimu wake huo wa kwanza.
Na kisha msimu wa pili Barca walibeba La Liga na kisha Dinho akachaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Dunia na wewe mwenyewe unaweza kuendelea na historia ya mafanikio ya mtakatiifu Gaucho.
So usikurupuke siku nyingine kufananisha Paa na Mbingu...