Georgia: Rais Salome Zourabichvili agoma kuachia Ikulu huku Mrithi wake akiapishwa

Georgia: Rais Salome Zourabichvili agoma kuachia Ikulu huku Mrithi wake akiapishwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Madaraka matamu sana usione Chairman anatoana kamasi na kibaraka wa Wazungu unadhani wanatania 🤣🤣🤣👇👇

1735553360146.jpeg

Mikheil Kavelashvili ambaye ni Rais mteule wa Georgia ameapishwa leo kuanza kulitumikia taifa hilo huku mtangulizi wake akigoma kutoka Ikulu ya taifa hilo.

Mikheil ameapishwa jana Jumapili Desemba 29, 2024, katika viwanja vya Bunge la taifa hilo Jijini Tbilisi, huku waandamanaji wanaomuunga mkono Rais anayemaliza muda wake, Salome Zourabichvili wakifurika mitaani.

Wakati Mikheil akiapishwa, Salome alikuwa akihutubia maelfu ya waandamanaji waliokusanyika nje ya Ikulu ya taifa hilo kuwa hamtambui rais mteule huyo kwa kile alichodai hakuingia madarakani kwa njia halali.

Kwa mujibu wa Salome, uteuzi wa Mikheil kama Rais wa taifa hilo ni batili mwa sababu wabunge waliompigia kura ya kuongoza taifa hilo wametokana na uchaguzi uliofanyika Oktoba mwaka huu uchaguzi ambao anadai uligubikwa na utata.
 
Halafu huyo Mikheil Kavelashvili ni mchezaji wa zamani wa Manchester City ya England na amepita katika klabu nyingi Ulaya...
 
Back
Top Bottom