Mwita25
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 3,831
- 1,169
Gerald Hando ameingia kwenye mgogoro na uongozi wa Clouds Radio baada ya kuonekana kwenye shoo iliyoandaliwa na Mbunge wa Mbeya mjini maarufu Sugu. Mtangazaji huyo wa kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast ameandikiwa barua ya onyo kali kwa kitendo chake ambacho kimekiuka sheria iliyowekwa hapo awali kuwa hatakiwi mfanyakazi yeyote kuhudhuria onesho hilo ambalo kimantiki lilipangwa kama muendelezo wa vita ya maneno kati ya Sugu na Clouds Radio. Hando hakuwa tayari kuelezea tukio hilo pale alipotafutwa kwa njia ya simu na mpekenyuzi wetu.
