Sheria gani hizo ambazo zinakinzana na katiba ya nchi,yaani kila mtu ana uhuru wa kwenda popote pale maadamu havunji sheria ya nchi na si sheria za Clouds,hayo mambo ni fikra duni haitakiwa yawepo katika ulimwengu wa sasa,sasa hawa clouds wangekuwa na uthubutu fulani wa dola si ingekuwa taabu,haya mambo madogo tu wanakomaa ,mambo mengine ni ya kibnafsi sana kumkataza mtu mzima na akili yake,je kama familia yake ilipenda iende huko na yeye akakataa si ndio mwanzo wa kuvunja amani katika familia,kitendo si cha uungwana kupingana kwa Clouds na Sugu kusiambukizwe na kwa watu wengine,demokrasia ni popote pale sio kwenye vyama vya siasa tu hata huko Clouds,heshimuni haki za wafanya kazi wenu hao ndio ng'ombe watoao maziwa