Usilaumu serikali kwa kila kitu. Jiulize wewe umechukua hatua gani ili upatiwe risti ambayo ni haki yako. Toka hapo kwenda TRA si mbali pia. Hii tabia ya kulalamika imewafanya watu wengine mshindwe kufuatilia mambo mengine ambayo yapo chini ya uwezo wenu. Sawa serikali imeonesha uzembe mkubwa wa kukusanya kodi lakini ni mara ngapi mmeambiwa kudai risti zetu mnapopewa huduma zenye kuhitaji kupatiwa risti au kufanya manunuzi.