Gereza la Segerea kuweni na utaratibu mzuri ili kupunguza msongamano wa watu

Gereza la Segerea kuweni na utaratibu mzuri ili kupunguza msongamano wa watu

Uwesutanzania

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2019
Posts
1,380
Reaction score
1,686
Kumekuwa na utaratibu ambao si rafiki sana wa muda ukifika gerezani hapo kwenda kumuona ndugu au jamaa yako mfungwa au mahabusu, kati ya mambo yanayopelekea sanasana uhatibifu wa muda eneo lile kwanza:-

Kuna baadhi ya watu huwa wanapewa masaa mengi zaidi kuonana na kuongea na wapendwa wao mle ndani hii inapelekea mlimikizano wa watu kuwa wengi nje unakuta kuna wakati inafikia watu mpaka 500 tunapigwa na jua.

Na pili ni kwenye kuandikisha majina yaani utakuta watu wamejazana hapo na waandishi wenyewe ni wawili alafu wapo slow kinyama. Wanaandika pole pole kama hawaioni ile foleni.

Tatu ambayo ni kero zaidi. Nipale unakuta watu wanakuja tu waongea na askari askari anawaleta moja moja pale kkwa wale madada waandishi wanaandikwa chap alafu wanaondoka na yule askari waliokuuja naye wanaenda angalia wapendwa wao.

Nilipojalibu kumuuliza jilani yangu mmoja akaniambia hao huwa wanaonga ela tena ni 1000 au hata 2000 yeye mwenyewe huwa anafanyaga hivyo ila tu leo kuna watu anawasubiri.

Tatizo la nne kwenye biashara inayouzwa pale ndani.

Yaani wanawawekeni kwenye foleni weee ili biashara zao ziende ambazo ni bei juu chai 300 kitumbua 500 soda ndo usiseme yaani ni shida tupu.

Ombi langu kwa wizara usika waanze kifuatilia utarabu wa pale ndani ili uwe rafiki kwa muda na kupunguza msongamano wa watu.
Shida iko nyingi pale ndani ila naomba niishie hapa.

-++--+-+++-+-+--+--+-+-+---+
 
We toa tu hiyo buku au buku mbili kwani utapungukiwa na nini jomba? Wape hivyo visenti Askari wakufanyie mpango tusiwe wanaa sana wakati uhalisia huwa hatuishi hivyo

Halafu chai sh 300 kikombe sio bei kubwa labda uwezo tumetofautiana
 
Umeeleweka poti, ila njaa zitawaua nyinyi.
 
Kuna mtu analazimishwa kunywa chai hapo,au ushirikina hutumika.
Mengine ht sio ya kuzungumza wewe ongea kero inatosha,swala la chai ni umbeya tu.
Litapoteza sura nzima ya malalamiko yako.
 
Ungewasilisha malalamiko yako kwa RSM angeyafanyia kazi hapa unapoteza muda tu!

Utaratibu huo upo Magereza yote, hakuna Gereza utaenda utakuta utaratibu mwingine
 
We toa tu hiyo buku au buku mbili kwani utapungukiwa na nini jomba? Wape hivyo visenti Askari wakufanyie mpango tusiwe wanaa sana wakati uhalisia huwa hatuishi hivyo

Halafu chai sh 300 kikombe sio bei kubwa labda uwezo tumetofautiana
kwahiyo wote tutoe buku buku si ndio?
 
We toa tu hiyo buku au buku mbili kwani utapungukiwa na nini jomba? Wape hivyo visenti Askari wakufanyie mpango tusiwe wanaa sana wakati uhalisia huwa hatuishi hivyo

Halafu chai sh 300 kikombe sio bei kubwa labda uwezo tumetofautiana

Unahamasisha rushwa??
 
Back
Top Bottom