Ndugu, Ukishaweka tangazo JF ni vizuri ukaamua kuwa muwazi kwa bei na kila kitu. Hakuna biashara ya uchawi hapa ambayo ni yule anayeloga tu anajua mbinu anazotumia. Kumbuka tunaishi kwenye zama gani. Kumbuka unatafuta soko na siku hizi ni soko huria. Mtu ana hiyari ya kununua au kutokununua toka kwako. Unapoweka mlolongo mrefu wa kutaka kujua nani yuko serious nani hayuko serious hii ni biashara kweli? Unaficha nini? Kama umeamua kuingia kwenye soko huria weka mambo wazi kila mtu ajue na aamue based on knowledge. Hujui unajizuilia wateja wangapi kwa kuweka mambo sirini! Ni ushauri tu
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.