Pre GE2025 Gerson Msigwa: Serikali yawahakikishia wananchi Uchaguzi Huru na wa Haki 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Moshi umeanza kufuka taratibu, maneno haya si mageni kwetu Gerson Msigwa. Hivi ndivyo Magufuli alivyosema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Uchaguzi 2020 - Rais Magufuli: Uchaguzi 2020 utakuwa huru na wa haki nini kilitokea?

Tunawalisha ng'ombe sumu kila siku afu eti tunategemea siku ya mnada hatutokuwa na vibudu, matokeo tofauti😹😹😹. Na wananchi hata hatuna tabu, tunakubali tu, si hatuna cha kufanya, 'tumefungwa mikono', hatuwezi furukuta, tumezibwa midomo hakuna neno hata moja latutoka!

====

Kwa upande wa serikali tumehakikisha mazingira yote ya kusimamia taratibu tulizojiwekea za uchaguzi yanazingatiwa na ndio maana tunafanya uchaguzi kwa amani na utulivu", Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa.

Amesema hayo leo Januari 2, alipokuwa akihojiwa Azam TV, Dar es Salaam.

Pia soma: Orodha ya CV za Wabunge kwa mwaka 2020 - 2025 kutoka kila mkoa Tanzania

Your browser is not able to display this video.
 
Wafanyie marekebisho ya haraka kwanza kwenye hiyo wanayo iita "Tume Huru ya Uchaguzi" ili iwe huru kweli! Kinyume na hapo, itakuwa ni vigumu sana kuyaamini maneno ya wanasiasa.
 
Waseme kwanza kama wameishiwa kura fake.
 
Ni afadhari usingeleta uzi huu wenye kichefuchefu!
 

Hii ni slogan ya kila mwaka
 
Msigwa huwa anavuta sigara gani?😡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…