Pre GE2025 Gerson Msigwa: Ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere umefika asilimia 99.80, mvua zisiponyesha hata misimu miwili bado tutazalisha umeme

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kusafirisha umeme ili kuhakikisha mikoa yote nchini inaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kwani kwa sasa, mikoa ya Katavi, Rukwa, Kagera, Lindi, na Mtwara ndio bado haijaunganishwa.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na wanahabari katika Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) mkoani Pwani siku ya Jumapili Februari 16, 2025.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema juhudi zinaendelea kuhakikisha maeneo haya yanapata umeme wa uhakika kupitia miradi inayotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Aidha ameeleza kuwa Mradi wa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) umeleta mabadiliko makubwa katika uzalishaji wa umeme nchini akieleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani Machi 2021, utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefikia asilimia 33. Hadi kufikia Februari 2025, maendeleo yamepanda hadi asilimia 99.80. Mashine nane kati ya tisa zimeshawashwa, na hivyo kuongeza MW 1,880 kwenye Gridi ya Taifa, hatua ambayo ameitaja kusaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini.

Aidha amesema kuwa serikali pia inaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa umeme ambapo Mradi wa kusafirisha umeme kutoka JNHPP hadi Chalinze wenye msongo wa kV 400 umefikia asilimia 99.5, ikilinganishwa na asilimia 44 mwaka 2021/22. Aidha kituo cha kupoza umeme cha Chalinze, ambacho ni sehemu ya mradi wa JNHPP, kwa sasa kimefikia asilimia 92 kutoka asilimia 35.9 mwaka 2021/22.

Mbali na JNHPP, Msigwa ameeleza kuwa miradi mingine ya umeme nchini inaendelea kutekelezwa kwa kasi ikiwamo mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo wenye MW 80 ambao umefikia asilimia 99.7 na tayari umeshaanza kuzalisha umeme, na Tanzania inanufaika na kiasi cha MW 27.

Mradi mwingine ni wa gesi wa Kinyerezi Extension wenye MW 185 ambao umefikia asilimia 97.6 na kwa sasa unachangia MW 160 katika Gridi ya Taifa. Mradi wa umeme wa Malagarasi wa MW 49.5, ambao wakandarasi wake walishapatikana, unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2027.

View attachment 3238263
Huyu alikuwa na hamu ya kulitaja jina la Daktari Samia Suluhu Hassani kulingana na maelekezo ya chama, matatizo ya umeme bado tunayo.
 
Msigwa ni mropokaji pia...angetulia tu....mambo ukame sio ya kufanyia siasa kamwe
 
Mbona hajamsifia wala kumtaja kiongozi mkubwa
 
Back
Top Bottom