Ubungoubungo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2008
- 2,502
- 741
Wajameni, naombe kueleweshwa, kwa sasa hivi, mozambique wanagundua gas nyingi sana karibia mara tatu ya hii tuliyogundua hapa tz, na wapo hadi karibia mpakani mwetu, yaani mto Ruvuma. pia kule ziwa Tanganyika wanasema kunaweza kuwa na mafuta na ziwa lile ni jembamba sana na mpaka upo katikati. swali langu ni kwamba, hivi haiwezekani tukaibiwa mafuta au gesi zetu na wenzetu aliotangulia au wakatu ule tunapokuwa tunachimba wote?
Mfano, Mozambique hawawezi kunyonya gas yetu kwenye visima karibu na mpaka wetu wakiwa kwao kule kule and vice versa?
Je, Congo na sisi hatuwezi kunyonyeana mafuta/gas kila mtu akiwa kwake?
Malawi na Tanzania hatuwezi kuibiana kila mtu akiwa kwake?
Au uchimbaji wake huwa unakuwaje kwa anayefahamu, mimi nikiwa pale mtwara siwezi kunyonya chini kwa chini gas iliyoko Mozambique au Wamozambique hawawezi kufanya hivyo wakiwa upande mwingine kule mpakani nasi?
Tukianza kuchimba, ni atakaye wahi ndio atafaidi au haiwezekani kuibiana?
Naongea hivi si ili kutaka sisi tuibe au kwamba tunawaonea wivu, hapana, naongea kwa nia nzuri tu ili kujua kama Mozambique wakitutangulia wanaweza kunyonya gas yetu ambayo vitalu vimekaribiana hata kabla sisi hatujajiimarisha kuichimba?
Maana kule Mozambique wamarekani wanataka kuingia ubia wajenge kituo cha kuprocess gas iwe processed tayari kuanza kuuza Asia na wametenga karibu $15 Billion. Please mwenye kufahamu hili naomba aniweke wazi ili nijue.
Thanks.