Gesi nyingine imevumbuliwa Bonde la Mto Wami

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
2,449
Reaction score
718
Wadau, juzi nimesafiri na ndugu mmoja, ni mtu mzima wa makamo, miaka sitini hivi na kuendelea.
Njiani tumeongea sana kuhusu kilimo na mashamba. Akasema ana heka hamsini ktk Bonde la Mto Wami, Mkoani Pwani ambako pia Vigogo kadhaa wana mashamba. Amesema kwa sasa wamezuiwa kulima na wanasubiri mchakato wa malipo ya fidia kwa maana imegunduliwa gesi, na ktk shamba lake Wagunduzi wameweka 'beacons' mbili ambapo vitachimbwa visima viwili.

Hizi habari nilikuwa sikuwahi kuzisikia awali, hivi miongoni mwenu wadau, wapo wanaofahamu uvumbuzi huu wa gesi ktk Bonde la Mto Wami?
 

Makampuni mengi ya uwekezaji hivi sasa yanahaha katika ukanda wote wa Pwani kusaka gesi na mafuta. Wameweka alama zao katika mashamba kadhaa kule Bagamoyo njia ya kwenda Mlandizi. Sina hakika na bonde la mto Wami lakini ndio ukanda wote huo wanatafuta.
 
Nani aliinusa hiyo ges mpaka kagundua?
 
afu mnasema tanzania kuna ardhi ya kumwaga check hii

eneo lote la mbuga za wanyama ni 25% ya total land area
madini ukiondoa gesi ni 15% ya total land area

bado huaweka maeneo ya gas.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…