diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
KAMPUNI 20 za ndani na nje ya nchi zimejitokeza kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya gesi asilia vya kuuza mitaani kwa jumla na rejareja kwenye vituo maalumu kama ilivyo kwa vituo vya mafuta. Kati ya kampuni zilizojitokeza kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta hiyo ni zile zenye vituo vya kujaza mafuta katika maeneo mbambali nchini.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mwezi uliopita kutangaza watu binafsi na kampuni zenye nia ya kuwekeza katika ujenzi wa vituo hivyo kujitokeza. Kaimu Meneja wa Biashara za Gesi katika TPDC, Dora Ernest alisema baada ya kupokea maombi hayo ambayo uwasilishaji wake ulikamilika Agosti 19 mwaka huu, watafanya uchambuzi kwa ajili ya kuwaita kuwapa utaratibu wa kufuata.
Alisema uwekezaji huo unafanyika katika maeneo inayopita miundombinu ya gesi katika mikoa ya Mtwara , Lindi na Dar es Salaam huku kukiwa na fursa lukuki katika upatikanaji wa gesi asilia kwa gharama nafuu na kila mahali. Hatua hiyo imetokana na TPDC katika mwaka huu wa fedha kuazimia kujenga vituo vikubwa viwili vya kuuza gesi asilia ili kuwezesha magari makubwa kubeba nishati hiyo kwa kutumia magari maalumu kisha kupeleka katika vituo na kwa watumiaji.
Alisema katika vituo viwili vikubwa vya kusambaza gesi hiyo asilia kwa wateja wa jumla ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM ) na kingine Muhimbili kitakachotumiwa pia na wafanyabiashara wa Feri na wataosambaza katika vituo vya kujaza gesi kama ilivyo kwa mafuta. “Wenye nia ya kuwekeza katika sekta hii lazima wawe na magari maalumu ya kubeba gesi (CNG trailer ), na wenye magari hayo wanaweza kuwa wasafirishaji tu mpaka vituoni, eneo kwa ajili ya mradi huo, uwezo wa kifedha, kitaaluma ili kumwezesha kufanya biashara hiyo,” alisema.
Alisisitiza kuwa maombi hayo yatapelekwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) itaangalia maombi hayo kisha ikiwemo vibali maalumu kama kile cha mazingira na mengineyo kisha kupatiwa leseni ili kuanza ujenzi. Alisema wanatarajia utekelezaji wa mradi huo kuanza Agosti mwakani wakati michakato yote itakapokamilika ya ujenzi wa vituo vya kuuza gesi huku wawekezaji wakikamilisha ujenzi wa vituo ili waweze kuchukua gesi na kusambaza.
Aliongeza kuwa, fursa hiyo inakwenda sambamba na fursa nyingine za kubadilisha mfumo wa magari kutoka mafuta kwenda gesi kufanyia matengenezo magari hayo na mengineyo ambayo vibali vyote vinapatikana EWURA.
“Unaweza kuona fursa zilivyo nyingi katika matumizi ya gesi asilimia , kwani kuna wataalamu watahitaika kwa wingi ambao ni wale wanaohakiki mifumo wa CNG kwenye magari ,ambapo kwa sasa nchini yupo mmoja tu,” alibainisha. Alisema licha ya kuwa Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), kinatarajiwa kusomesha wawili na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam watatu, bado kuna fursa za kusomea katika eneo hilo kwa wale wanaotaka, kwani kwa ukanda wa Afrika Mashariki mitihani yake hufanyika nchini Uganda.