Gesi tumboni

faby

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2011
Posts
2,214
Reaction score
767
Habari wakuu nasumbulia na maumivu ya gesi tumboni chini ya chembe.nitumie nini nijisikie nafuu!
 
>Pole sana mkuu.

Jaribu kupekua zaidi kwani kuna nyuzi nyingi zinazohusu tatizo hili.



>kwakukusaidia,
Kutokana na maelezo yako inaonesha unatatizo la Amoeba.

>Ebu nijulishe kama gesi inaambatana na dalili baadhi kati ya hizi hapa chini:
.Kujisaidia kinyesi chenye kamasi
.kukosa hamu ya kula
.Kujisaidia kinyesi mvilingo (kinachokatikakatika kama cha mbuzi)
.
.
.


DAWA
>METRONIDAZOLE
Hii ni dawa inayopatikana kwenye maduka ya dawa.

NOTE: Ni vyema kufanya vipimo vya kitabibu klabla ya kutumia dawa yoyote.
 
Nashukuru sana T.M
 
naomba nikuulize unapata gesi wakati gani ukinywa maziwa au ukishakula?au una gesi tu kwenye tumbo?
 
KULA HIVI KUONDOA MATATIZO YA TUMBO KUJAA.


Mtindi



Papai

KWA njia moja au nyingine, unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie. Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo.

CHANZO

Kabla ya kukimbilia kwenye tiba, ni vizuri kwanza kujua chanzo cha tatizo na katika hili unahitaji kujua ni vyakula gani ukila vinasababisha matatizo ya tumbo. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo.
Kwa mujibu wa Mkurugezni wa Tiba wa Chuo Kikuu cha Tolune. DK. Timothy S. Harlan (M.D) ambaye pia anajulikana kwa jina la utani kama Dk. Gourment, vyakula na vinywaji vinavyochangia tumbo kujaa na ukosefu wa choo kwa muda mrefu huwa ni soda, ulevi (hasa bia), vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye chumvi nyingi.
Kwa mujibu wa Dk. Harlan, vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakula na uondoaji wa uchafu kwenye utumbo, hivyo huwa kikwazo katika mfumo mzima wa usagaji chakula kwa urahisi.
Ili kujiepusha na matizo ya tumbo ya muda mrefu na hata kuzuia uwezekano wa kuumwa na tumbo mara kwa mara, unashauriwa kula vifuatavyo, karibu kila siku ili kulifanya tumbo lako kuwa safi wakati wote:


PAPAI (PAPAYA)

Baadhi ya utafiti uliyopo, unaonesha kwamba ‘enzyme’ waliyomo kwenye papai husaidia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kulifanya tunda hili kuitwa na mtafiti wa zama za kale Christopher Columbus kama ‘tunda la malaika’.
Watafiti wamebaini kuwa tunda hili, lenye ladha tamu na harufu nzuri, huboresha mfumo wa usagaji chakula, husafisha utumbo, huzuia magonjwa ya uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.
“Vitamini na virutubisho vya papai vina faida nyingi, lakini faida kubwa ya papai ipo kwenye kirutubisho (Enzyme) aina ya ‘Papain’ ambacho hujulikana kwa uwezo mkubwa ilionao wa usagaji mzuri wa chakula tumboni,” anasema Dk. Cari Case mwandishi wa blog ya masuala ya afya.

Mwandishi huyo anaongeza kwa kusema kuwa papai limekuwa likitumika kama tiba tangu karne ya 18, lakini utafiti wa kisayansi haukugundua faida za papai hadi mwaka 1870 wanasayansi walipogundua kirutubisho cha ‘papain kilichomo kwenye papai na tangu wakati huo tafiti nyingi zimekuwa zikifanywa kuhusu faida za tunda hili na uwezo wa tiba iliyonalo.

MTINDI (YOGURT)

Hata kama wewe si mpenzi wa mtindi, jaribu kunywa na utaupenda, hasa uwezo wake wa kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Mtindi mzuri ni ule ‘plain’ ambao haujachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza ladha. Bakteria asilia waliyomo kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mwepesi.
Mwisho, ili kupata faida ya papai na mtindi kama ilivyoelezwa hapo juu, ni vizuri ukala mara kwa mara kama siyo kila siku, kabla au mara baada ya kula vyakula ambavyo vinaweza kukuletea shida tumboni, au ukaweka mazoea ya kula kila siku ili kuliweka tumbo lako katika hali salama.
 

Attachments

  • Papayaenzymedigestion.jpg.jpg
    16.8 KB · Views: 3,620
Je,mh. Mzizi Mkavu mtindi kwa mwenye 'ulcers' hauna madhara?
Mtindi hauna madhara ya vidonda vya tumbo.Mkuu@Vegetarian

VYAKULA TIBA KWA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO




Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine', vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

ULAJI CHUMVI

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.


MAFUTA YA SAMAKI

Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.


VITAMINI NA MADINI

Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO

Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha
 
Habari umundani Mimi Nina matatizo ya Gasi ndio majibu nilio pewa baada kipimo cha ENDOSCOPY mana Nina dalili zifuatazo, kkichwa kuuma kidogo Sehem Ie Vidonda vya tumbo vinaumisga mgongo Mpaka Kiuno Mara koromeo inabanwa mkono n.a. mkuu kama vile vinataka kupooza kichwano najiskia kama Nataka kuchuzika vile je hizo dalili ndivyo anavyo JISKIA MGONJWA WA GASI AO VIDONDA VYATUMBO.
 
Labda kwa wengine mimi nikila vyakula mlivyosema hapo tatizo la gesi linakuwa mara 1000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…