Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Bado nasimamia kwamba Trump na Netanyahu wamechanganyikiwa kuhusiana na wapalestina na hasa Hamas. Wanapenda na wangetamani vita vingekwisha na kutangaza ushindi.Jambo hilo ni gumu kwa sasa na Hamas wameganda bado huko Gaza.
Katika nyakati tofauti raisi Trump na mwenzake huyo wametoa matamshi mabaya kustahiki kutolewa na binadamu kwa binadamu mwenzake,kwamba iwapo Hamas hawatawaachia mateka wote na wao kutoonekana Gaza basi watafungua geti la jahanamu (Gate of hell).
Trump kwa kiburi alipohojiwa kuhusu kitisho hicho akaongeza kwa kusema hilo litatokea na Hamas watajua anachokusudia.Kuonesha kuwa Netanyahu ana nia na mawazo kama ya Trump na yeye naye akasema yuko njiani kutekeleza mpango huo wa Trump.
Cha muhimu ni kuwa watu wawili muhimu kusaidia mpango huo ambao Trump kwa kigezo cha misaada inayotoa kwao wangekubali na wao wamepinga mpango huo na kuonesha dalili za kutokuwa tayari kusaidia ufunguzi huo wa geti la Jahanamu.
Mfalme Abdullah alitoa kauli ya kupinga kuhamishiwa wapalestina nchini kwake hadharani alipokwenda kukutana na Trump huko Marekani.Elsisi wa Misri kwa upande wake amesema iwapo hoja ni kuijenga Gaza baada ya kubomolewa basi hilo lifanyike bila kuhamishwa mtu yoyote.
Katika hali hiyo viongozi hao madhalimu wa Marekani na Israel watakapoendelea na njama hizo basi waangalie sana kwani geti hilo lina dalili kubwa la kufungukia upande wao pia.
Watu wa mataifa mbali mbali watapinga kitendo hicho na kusababishwa kutengwa kivitendo kwa Marekani na Israel.Kwa upande wa mataifa ya kiarabu na ya kiislamu hawatakuwa tayari kuona wapalestina wakiuliwa kama mwanzo.
Waarabu hao watapanda hamasa sana wakiona wapalestina wa Gaza wakisakwa na kupakiwa kwenye malori kupelekwa wasikokujua kutoka ardhi zao.
Kwa upande wa Muumba mbingu na ardhi kwa mara nyengine anaweza akafungua lango hilo upande wa Marekani na Israel kwa mfano wa kilichotokea Los Angels miezi miwili iliyopita na kama vile ilivyotokea huko nyumba kama ilivyoandikwa kwenye tariikh.