Geti la upana futi kumi linaweza kuleta shida kupita gari ndogo?

Geti la upana futi kumi linaweza kuleta shida kupita gari ndogo?

Udochi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2015
Posts
787
Reaction score
1,056
Wakuu,

Jirani yangu ameniambia kuwa geti langu la futi 10 linaweza kupelekea gari kugonga nguzo wakati wa kuingia au kutoka.
Hii ni kweli?

Kwa sasa sina gari, Ila naomba mnipe uzoefu kabla sijaingia gharama ya kubomoa nguzo ili kuongeza upana wa geti kwa ajili ya matumizi ya baada'e.
 
Gari litapita vizuri Ila itakupasa kulifungua geti zima
 
10ft ni kama 3m, gari ndogo nyingi ni 1.5-2m upana. Gari kubwa malori hakuna inayozidi 3m upana pia maana hata baadhi ya barabara zetu lanes zake hazifiki hata 3m baadhi ya barabara za lami kabisa. Angalia tu kama sehemu ya kuangalia na kutoka kwenye geti una nafasi ya kutosha, kama ipo usipoteze pesa yako kubomoa chochote.
 
Back
Top Bottom